Muwakilishi wa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wa Gana: Iraq ni nchi ya kijamii na watu wake wameithibitishia dunia kushikamana kwao na Marjaa dini mkuu na kuitikia fatwa yake..

Maoni katika picha
Shekh Ahmad Kamalidini Abuu Bakari kiongozi wa jamii ya shia katika jamhuri ya Gana amesema kua: “Iraq ni nchi ya kijamii na watu wake wana maadili mema, wameuthibitishia ulimwengu kushikamana kwao na Marjaiyya tukufu na kuitikia fatwa zake, hili si jambo geni kwa watu wanao jitambua kama watu wa Iraq, leo hii vijana wao wanaendesha vita kali dhidi ya magenge ya magaidi kwa niaba ya ulimwengu mzima, kwa utukufu wao ardhi imekombolewa na maeneo matukufu yamesalimika”.

Akaongeza kusema kua: “Watu wa Iraq wanaipenda nchi yao, wamepigana kwa ujasiri wa hali ya juu kabisa na kujitolea muhanga, kama si kujitolea kwao muhanga na damu tukufu zilizo mwagika katika ardhi hii, Iraq isinge kombolewa kutoka mikononi mwa magaidi, mimi nimetembea katika nchi nyingi za kiarabu lakini Iraq ndio inawatu bora zaidi, wakarimu na wanaopenda maendeleo, tuliyo yaona katika miradi ya Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) ni dalili ya wazi kwa haya ninayo sema”.

Amasema kua: “Kongamano la Rabiu Shahada ni zuri sana na linastahili kuitwa kongamano la kimataifa, kuanzia ubora wa mpangilio wake, mambo yaliyomo katika kongamano, aina ya wageni washiriki wanatoka nchi tofauti za kiarabu na kiajemi, ukizingatia kua kongamano hili linahuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa nuru za Muhammad, shukrani za dhati zimuendee kila aliye changia kufanikisha kongamano hili tukufu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: