Kama ushiriki wake katika maonyesho yaliyo pita ya vitabu ya kimataifa Karbala, Atabatu Abbasiyya tukufu inasifika kwa kua na machapisho mbalimbali katika matawi yake yanayo shiriki maonyesho.
Ataba tukufu ambayo pia ni mlezi wa maonyesho haya imeshiriki kupitia matawi mengi ambayo ni:
Kwanza: Tawi la kitengo cha habari na utamaduni, lina machapisho mbalimbali ya vitabu vikubwa na vidogo vyenye maudhui tofauti za kidini, tabia njema, malezi pamoja na maudhui za kisekula, vikiwemo na vitabu vilivyo fanyiwa uhakiki na kuchapishwa katika muonekano mpya miongoni mwa vitabu vyenye umri mkubwa zaidi.
Pili: Tawi la maarifa ya kiislamu na kibinadamu, tawi hili lina machapisho na matoleo ya vituo vilivyo chini yake (kituo cha turathi za Karbala, Hilla na Basra), ukiongeza na machapisho yake, kama vile machapisho yanayo husu Qur’an tukufu, yanayo tolewa na Maahadi ya Qur’an ambayo ipo chini yake, na miongoni mwa machapisho hayo ni msahafu uliochapishwa na Atabatu Abbasiyya hivi karibuni.
Tatu: tawi la kitengo cha zawadi na nadhiri, wameshiriki kwa kuonyesha vitu wanavyo tengeneza kutokana na fedha kama vile pete, pia vipande vya marumaru za nakshi na vitambaa vilivyo dariziwa na vinginevyo.
Nne: Tawi la uchapishaji, Daru Kafeel ya uchapaji na usambazaji, wameshiriki kwa kuonyesha baadhi ya vifaa vyao wanavyo vitumia katika uchapaji.
Tano: Tawi la idara ya watoto na makuzi chini ya kitengo cha habari na utamaduni, wao wameonyesha vifaa vya watoto, majarida, vifaa vya kusomea, na vitu mbalimbali vya watoyo wa kiume na wakike.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imeshiriki katika maonyesho na makongamano mengi ndani na nje ya Iraq, hupata mwitikio mkubwa kutoka kwa wadau, katika kila maonyesho hua na machapisho mapya tofauti na nyingine.