Mwakilishi wa nchi za Ulaya wa zamani katika mashariki ya kati: Nimekuta alama za uadilifu kwa Imamu Hussein (a.s)..

Maoni katika picha
Mwakilishi wa zamani wa nchi za umoja wa Ulaya katika mashariki ya kati na mkuu wa tume ya maelewano ya kimataifa bwana Alistar Krouk amesisitiza kua: “Nimekuta alama za uadilifu kwa imamu Hussein (a.s)”.

Aliyasema hayo katika ujumbe aliotoa kwenye hafla ya kuhitimisha kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu iliyo fanyika alasiri ya Alkhamisi (7 Shabani 1438 h) sawa na (4 May 2017 m), miongoni mwa aliyo sema ni: “Kongamano la Rabiu Shahada ni kongamano kubwa linaendana na mnasaba mkubwa zaidi, ninatoa shukrani kwa kila aliye changia kufanikisha kongamano hili hususan uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), ambao wameonyesha umuhimu mkubwa sio katika kongamano hili tu, bali napenda kuwashukuru sana kwa huduma wanazo toa mfululizo kwa watu wanao kimbia mateso ya magaid ya Daesh, nimeshuhudia huduma zinazo tolewa na Ataba hizi kwa wakimbizi”.

Akabainisha kua: “Siku ambazo nimekuwepo katika eneo hili tukufu nimeathirika sana, mambo yote niliyo shuhudia yamebaki katika akili yangu, nitaenda kusimulia nikirudi Ulaya, nimepata imani katika ziara hii na nimeona mazingira ya imani kwa watu wanaokuja kufanya ziara katika eneo hili tukufu, walikua na msukumo mkubwa wa imani kama vile kuna nguvu inayo wasukuma katika imani”.

Akasema kua: “Najafu Ashrafu, Karbala tukufu na mji wa Kufa ni vituo vya mwanga wa uislamu, na zitarejea katika nafasi yake ya zamani, waislamu wa Iraq wana uwezo mkubwa na wanajiamini, huu ni ujumbe kwa wote, maendeleo niliyo yaona katika Ataba ni dalili ya wazi ya uwezo walio nao na ujumbe huu nitaufukisha Ulaya”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: