Kamati ya usimamizi wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa Karbala yatoa zawadi kwa vituo vilivyo shiriki na yavitaka kushiriki tena katika maonyesho yajayo..

Maoni katika picha
Pembezoni mwa kongamano la Rabiu Shahada la kitamaduni na kimataifa awamu ya kumi na tatu, asubuhi ya Ijumaa (8 Shabani 1438h) sawa na (5 May 2017m) katika ukumbi wa Sayyid Auswiyaai (a.s) ndani ya Atabatu Husseiniyya kumefanyika hafla ya kufunga maonyesho ya vitabu ya kimataifa yaliyo fanywa chini ya kauli mbiu isemayo (Ili tusome pamaoja) yaliyo dumu kwa wiki mbili, na kutoa zawadi kwa washiriki wa ndani na wakigeni.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ukafuata ujumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano ulio tolewa na Sayyid Afdhal Shami rais wa kamati hiyo na msaidizi wa katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya tukufu, alitoa shukrani kwa taasisi na vituo vyote vilivyo shiriki katika maonyesho haya ya vitabu na kwa kuitikia mwaliko walio pewa.

Akaongeza kusema kua: “Kama mlivyo ona mwaka huu washiriki wametoka nchi tofauti, kuna nchi (35) zilizo shiriki katika kongamano hili kutoka mabara yote, kongamano hili hufanywa kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa maimau watakasifu na kuangazia historia yao, hali kadhalika kwa ajili ya kuwasiliana na walimwengu, Mwenyezi Mungu mtukufu ameumba watu makabila na mataifa ili wapate kujuana, kujuana huko kuna faida nyingi kwa wote, napenda kuzungumzia nukta mbili, ya kwanza: Nawapongeza ndugu zangu watukufu waliokuja katika mji wa Karbala na wameishi pamoja na watu wa mji huu, nawaomba wawe mabalozi wa kuelezea sura halisi waliyo ishuhudia katika mji huu, kwa masikitiko makubwa jambo kubwa linalo kumba jamii za kiarabu kwa sasa ni imani kali za kidini, naamini kila aliye ingia katika Ataba aliswali namna atakavyo wala hakuna aliye muhoji wala kumshangaa.

Nukta ya pili ni: Yanayo tokea Sirya, Iraq, Libia na nchi zingine za kiarabu kutokana na imani kali, hivyo ni jukumu la waungwana wote katika nchi za kiarabu na kiislamu wakemee imani kali za kukufurishana na uharibifu unaofanywa.

Ukafuata ujumbe wa wizara utamaduni ya Misri, ulio tolewa na muwakilishi wa wizara hiyo dokta Muhammad Fairuzi, alianza kwa kuzishukuru Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) kwa kuendesha makongamano ya kitamaduni, akasema kua: “Hakika jambo hili linaonyesha kupevuka, uislamu ni dini na dunia na elimu na utamaduni (maadili mema) vinamfanya mwanadamu asidumbukie katika dimbwi la ujinga, tumejiridhisha kua Iraq ni nchi ambayo watu wake wanahurumiana, watu wa Iraq hawabaguani, natoa shukrani za dhati kwa watumishi wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) ambao wametoa huduma bora kabisa kwa wageni na kwa uaminifu mkubwa".

Kisha ukafuata ujumbe wa vituo vya usambazaji vilivyo shiriki katika maonyesho, ulio tolewa na Ustadh Swalaah Talawiy, mjumbe wa muungano wa wasambazaji wa vitabu wa Jodan, ambaye alisema kua: “Hakika ni wajibu wa wasambazaji wa vitabu wa kiarabu na kiislamu kupambana na fikra za chuki kutokana na kinacho zikumba nchi za kiarabu, huu ni wajibu wa msambazaji yeyote popote atakapo kua, ukizingatia kua uwanja huu mtukufu –Maonyesho ya vitabu ya kimataifa ya Karbala- yanasaidia kuziweka karibu dini, mataifa na madhehebu zote, ni fahari kwetu kupata nafasi ya kushiriki katika kongamano hili tukufu”.

Hali kadhalika mkuu wa maonyesho ya vitabu ya kimataifa ya Karbala Sayyid Muyassir Hakeem alisema kua: “Maonyesho ya vitabu ya kimataifa ya Karbala awamu ya kumi na tatu yaliyo fanyika katika aridhi hii tukufu, yametukutanisha na wasambazaji wapya na vitabu vyenye maudhui tofauti na machapisho mapya, maonyesho haya ni sehemu ya ratiba ya kongamano la Rabiu Shahada, Ataba za Iraq zinatilia umuhimu sana jambo la usambazaji wa vitabu na utamaduni, tamaduni ni msingi wa kuundwa kwa mataifa na chanzo cha utulivu na amani, kusambaza utamaduni ni wajibu wa kila msambazaji na wakuu wake, serikali, taasisi na jamii, hivyo kulikua na harakati maalumu iliyo fanywa na kamati ya maonyesho ya vitabu kwa kwenda nchini Misri na kukutana na viongozi wa wizara ya utamaduni pamoja na kamati kuu inayo husika na mambo ya vitabu, na kuwaelezea kwa kina ratiba ya kongamano na maonyesho, hali kadhalika ushirikiano tulio nao wa moja kwa moja na wasambazaji wa vitabu wa Lebanon na Jodan, natarajia mwaka huu uwe kama miaka ya nyuma sisi sote tutoke na kutu fulani”.

Hafla ilihitimishwa kwa kutoa zawadi kwa washiriki wa maonyesho ya vitabu wa kitaifa na wakigeni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: