Mu’utamad Marjiiyyah dini mkuu katika mji wa Karkuki Sayyid Qambar Mussawiy amesema kua: “Kuja kwa wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) na washirika wao kuukomboa mji wa Bashiri walitutua mizigo iliyo kua migongoni kwetu, na walifungua minyororo ya utumwa katika nyoyo zetu kabla ya kukomboa aridhi yetu, na walitutia nguvu na kutupa matumaini ya kinacho weza kutokea baadae, Mwenyezi Mungu atuepushie”. Hayo aliyasema katika kongamano lililo fanywa Juma Pili (10 Shabani 1438h) sawa na (7 May 2017m) katika mji wa Bashiri kwa mnasaba wa kumaliza mwaka tangu kukombolewa kwake.
Akaongeza kusema kua: “Hakika mtihani tulio pata katika mji wa Bashiri ulitufundisha mambo mengi na ukatuthibitishia kua hatuko pekeyetu, bali nyie wote mko pamoja nasi, tulipo baini hilo unyongo uliondoka, uzuri ulioje wa neno hili! hapo awali hamkujua kama mnandugu zenu katika mji wa Bashiri, katika mji huu yamechanganyika machozi ya wazazi wa mashahidi na damu za mashahidi miongoni mwa vijana wa Basra, Naswiriyya, Ammaara, Samaawa, Dinaawiyya, Najafu, Karbala, Bagdadi na mikoa yote, ikatengenezeka nguvu ya ushini na ikawa ni tiba kwa wenye maradhi”.
Akabainisha kua: “Nyie ni ngao na ngome yetu tumepata nguvu kwa ajili yenu leo, kesho n ahata siku zijazo, amani iwaendee mashahidi wote hususan walio pata shahada katika aridhi ya Bashiri, amani mara elfu kwa kila mpiganaji aliye simama kwa utukufu, bila shaka damu zilizo mwagika katika aridhi ya Bashiri zinaweza kuunganisha safu zetu na kauli zetu mbele ya adui, tukasimama mbele yake tukiwa kitu kimoja na nguvu moja.