Mwakilishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu: Tumekuja na kikosi hiki kinacho jifunza ujasiri kutoka kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) kupandisha pendera ya ushindi na kushirikiana nanyi katika furaha..

Maoni katika picha
“Tumekuja na kikosi hiki kinacho jifunza ujasiri kutoka kwa Abulfadhi Abbasi (a.s) kupandisha bendera ya ushindi na kunusa harufu ya maua ya kujitolea muhanga, ya damu tukufu iliyo mwagika kwa ajili ya ubinadamu”, haya yalisemwa na Shekh Kamaal Karbalaiy katika ujumbe aliotoa kwaniaba ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika kongamano lililo fanywa alasiri ya Juma Pili (10 Shabani 1438h) sawa na (7 May 2017m) katika kitongoji cha Bashiri la kusherehekea kumaliza mwaka toka kukombolewa kwake.

Aliongeza kusema kua: “Enyi ndugu watukufu tumekuja kutoka katika aridhi ya Hussein Shahid, aridhi ya mawasii, aridhi ya Abulfadhil Abbasi (a.s), aridhi ya kujitolea muhanga, kutoka katika madrasa ya kudumu iliyo toa makomando na kutengeneza watu majasiri vizazi na vizazi, tumekuja kuwapongeza kwa ushindi mlio pata, ulio jaza furaha kwa wakazi wa Bashiri, na kuwakumbusha katika mwaka huu mpwa damu tukufu zilizo jifunza muhanga kwa Sayyid Shuhadaa na maimamu watakasifu, walio mkomboa mwanadamu kutoka katika unyama hadi katika ubinadamu halisi, kujitolea kwao kuliwatoa watu katika shirki na kuwaingiza katika tauhid, na katika ukafiri hadi katika imani, na katika upotovu hadi kwenye uongofu, tumekuja kuwakilisha Marjiiyya tukufu na Atabatu Abbasiyya, kutoka katika aridhi takatifu, bila kumsahau kiongozi wake mkuu wa kisheria na katibu mkuu pamoja na watumishi watukufu wote, tumekuja kusherehekea pamoja na nyie”.

Akaendelea kusema kua: “Katika muda huu ambao tunaona ushindi ukizaa ushindi mwingine, Marjiiyya watukufu wanawataka muendelee kuenzi ushindi huu, hadi haki itakapo shinda, na kuendelea kuhami maeneo matukufu. Enyi watu wa Bashiri mlipata matatizo mengi kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu na mtume wake (s.a.w.w) mliyashinda, ewe Swahibu Zamaan tunakupongeza kwa ushindi huu, unaziona nyuso hizi tukufu tunakuomba unusuru dini hii na waumini hawa, na uwaokoe kutokana na maadui wa dini, tunamuomba Mwenyezi Mungu kwa utukufu wako adumishe ushindi huu na ailinde nchi hii, na tunatarajia kua wanajeshi watiifu chini ya bendera yako tukufu”.

Akafafanua kua: “Enyi ndugu zangu, kikosi cha Abbasi (a.s) kimejitolea nafsi zake kwa ajili ya kuwalinda na kulinda maeneo matukufu, wameshirikiana nayi kwa kutoa mashahidi na kumwaga damu, wala sioni ispokua roho za waja wema zikipepewa katika aridhi hii tukufu wakishirikiana nanyi kusherehekea ushindi huu, kila ushindi utazaa ushindi inshallah”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: