Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya nadwa kuhusu fatwa ya kujilinda na nafasi yake katika kuishi kwa amani na athari yake kijamii..

Maoni katika picha
Miongoni mwa kongamano la kutekeleza ahadi linalo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kituo cha (Ameed duwaliy lilbuhuthi wa dirasaat) kwa kusaidiana na chuo kikuu cha Karkuki asubuhi ya Juma Tatu (11 Shabani 1438h) sawa na (8 May 2017m), wamefanya nadwa kuhusu fatwa tukufu ya kuilinda Iraq na maeneo matakatifu pamoja na athari yake katika jamii ya wairaq, nadwa ilifanyika katika ukumbi wa chuo kikuu cha Karkuki chini ya kauli mbiu isemayo (Kujilinda kutukufu na kuishi kwa amani) kwa kushiriki watafiti wa kituo cha Ameed na chuo cha Karkuki, nadwa ilipata mahudhurio makubwa kutoka nje ya chuo pamoja na walimu na wanafunzi wa chuo hiki.

Nadwa ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq halafu ukaimbwa wimbo wa taifa, ukafuata ujumbe wa kikosi cha imamu Ali (a.s) cha wapiganaji, ulio wasilishwa na Sayyid Ali Shar’I kutoka katika Atabatu Alawiyya tukufu, miongoni mwa aliyo sema ni:

“Mwenyezi Mungu mtukufu ametuneemesha neema kubwa sana ambayo hailinganishwi na neema yeyote, nayo ni neema ya Marji’iyya wakuu, ambao wamehifadhi nchi, raia na wamelinda umoja na mshikamano wa jamii ambayo maadui walikusudia kuigawa, lau kama sio hekima ya Maraajii wetu watukufu kupitia maelekezo yao ya ubaba yamesaidia sana kutuliza hali ya uhasama, na fatwa tukufu ya kujilinda iliyo amsha makundi kwa makundi ya vijana”.

Halafu ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Ustadh Maitham Zaidiy ambaye alisema kua: “Miongoni mwa furaha na fahari yetu ni kuhudhuria katika tabaka la watu wenye elimu ambao wanatunza historia na kutengeneza mustaqbali, katika chuo hiki kitukufu na mji mzuri ambao unahifadhi wakimbizi wengi na umelinda heshima ya wairaq kinasaba au kidini na kadhalika, tunashuhudia kongamano linalo fanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kuhusu kukombolewa kwa mji wa Bashiri, mji uliokua umedhulumiwa, likibeba anuani ya (Ukombozi wa mji wa Bashiri unatengeneza umoja wa taifa), anuani hii ina athari kubwa sana na pengine ni ponyo kwa wenye majeraha, Marji’iyya wanasisitiza sana umoja na mshikamano wa wairaq pamoja na kuilinda nchi yetu, hatuna kitu kingine zaidi ya Iraq, hiyo ndio ngao yetu imara, kupitia hotuba zao mbalimbali. Matatizo yanayo tokea katika nchi hii yanatokana na kuingiliwa na mataifa ya nje, uingiliaji wowote wa mataifa ya nje hauna maslahi kwa taifa letu, kwani wao wanataka mali za Iraq tu, ni jukumu letu kushikamana na kulinda taifa letu kama tulivyo shikamana katika kukomboa mji wa Bashiri na tukapata mashahiti kutoka mikoa yote ya Iraq na katika tabaka zote za wairaq”.

Pia kulikua na ujumbe wa chuo kikuu cha Karkuki ulio wasilishwa na dokata Hassan Abbasi, alisema kua: “Wamefaulu mashahidi wetu watukufu walio jitolea kwa ajili yetu, kama sio wao tusinge weza kuendelea kutoa elimu katika chuo chetu, na kusinge kua na uhai katika mji huu, mji wa Karkuki unaenzi kuishi kwa amani”.

Kikao kikaingia sehemu ya pili ambayo jumla ya watafiti watano waliwasilisha kati zao kama ifuatavyo:

Mtafiti wa kwanza: Dokta Sarhani Jafaati, utafiti wake unahusu (Amani ya kijamii nchini Iraq) alifafanua kuhusu athari zilizo sababishwa na Daesh walipo ingia Iraq na namna ya kupambana nazo ili kuleta amani katika jamii ya wairaq kwa mujibu wa mtazamo wa Marji’iyya dini wakuu na maelekezo yao.

Mtafiti wa pili: Dokta Aadil Nadhir kutoka katika kituo cha Ameed cha kimataifa, utafiti wake unahusu (Mtazamo wa usia wa Sayyid Sistani kwa wapiganaji) alielezea kuhusu usia wa Sayyid Sistani (d.i.w) kwa wapiganaji.

Mtafiti wa tatu: Ustadh Haidari Ghaazi Mussawiy, aliandika kwa lugha ya kiengereza, utafiti wake ulihusu (Swala ya Ijumaa ni faradhi kuu (asilia) au ni faradhi elekezi kwa mujibu wa mtazamo wa hakika na ahadi) alielezea nafasi ya Marji’iyya katika kuanzisha kambeni ya kuishi kwa amani na usalama kwa wananchi wa Iraq.

Mtafiti wa nne: Dokta Aamir Aashuur kutoka chuo kikuu cha Karkuki, utafiti wake unahusu (Nafasi ya vyombo vya habari katika kampeni ya kuishi kwa amani na kupambana na fikra za kukufurishana na ugaidi) alielezea matatizo mengi yanayo ikumba jamii ya wananchi wa Iraq na nafasi ya vyombo vya habari katika kubainisha fikra botofu zinazo zaa ugaidi na msimamo ya katiba ya Iraq.

Mtafiti wa tano: Omari Najmu kutoka chuo kikuu cha Karkuki, utafiti wake unahusu (Kuishi kwa amani na nafasi yake katika kujenga familia) alielezea nafasi ya familia katika kujenga jamii salama.

Nadwa ilihitimishwa kwa kumpa zawadi mkuu wa chuo na washirika wake walio andaa nadwa hii pamoja na wataalamu walio wasilisha tafiti zao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: