Waziri mkuu dokta Haidari Abadi atembelea Atabatu Abbasiyya tukufu na akutana na kiongozi mkuu wa kisheria..

Maoni katika picha
Kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi (d.i) siku ya Juma Tatu (11 Shabani 1438h) sawa na (8 May 2017m) amempokea muheshimiwa waziri mkuu dokta Haidari Abadi katika ziara ambayo ni miongoni mwa utekelezaji wa majukumu yake ya kiserikali kuhusu Ataba tukufu.

Dokta Haidari Abadi yupo katika ziara ya Ataba tukufu za Karbala, alipokewa na katibu mkuu Sayyid Ashiqar (d.t) na jopo la viongozi wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Kumbuka! waziri mkuu alifika kabla ya leo katika mji wa Karbala na akatembelea malalo ya Sayyid Shuhadaa imamu Hussein (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: