Tawi la Atabatu Abbasiyya tukufu limepata mwitikio mkubwa katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa mjini Tehran awamu ya thelathini, yanayo fanyika katika mji wa Shamsi – Shahru Aftaab kusini ya mji mkuu wa Tehran, kutoka kwa watu wanao tembelea maonyesho hayo, limekua kivutio kikubwa kwao, kutokana na bidhaa walizo nazo kukidhi mahitaji yao kitamaduni na kielimu pamoja na mvuto wa banda lao lililo tengenezwa kwa umaridadi mkubwa huku likifanana na jengo la malalo ya Abulfadhi Abbasi (a.s) likiwa na umbo la kubba tukufu lenye bendera.
Miongoni mwa watu wazito walio tembelea tawi hilo ni pamoja na; Mgombea urais wa Iran na waziri wa utamaduni wa zamani Mustwafa Miri Salim, walipewa maelezo kwa ufupi kuhusu bidhaa za Ataba na namna wanavyo chapisha na kutoa vitabu hivyo katika muonekano mzuri, mwisho wa ziara yao walisema kua: “Hakika kushiriki kwa Ataba tukufu katika maonyesho haya ya kimataifa kunastahili sifa kubwa na kujivunia swala hilo”.
Naye waziri wa utamaduni wa Iran na mkuu wa maonyesho haya Ridhwa Swalehi Amiriy walitembelea tawi la Ataba na wakasifu ushiriki wao na wakasema hii ni fursa muhimu ya kutambuana na kujenga uhusiano.
Tawi hili limetembelewa na watu wengi wazito, wakiwemo walimu wa hauza, walimu wa vyuo vikuu na wasomi wa kisekula, wote walivutiwa na vitabu vilivyopo katika banda letu na wakaomba ushiriki wetu uendelee katika maonyesho haya.
Kumbuka kua hii ni mara ya nane kushiriki Ataba tukufu katika maonyesho haya ambayo yanafanyika mwaka huu kwa awamu ya thelathini, Ataba imeshiriki ikiwa na aina zaidi ya mia mbili (200) za vitabu mbalimbali na majarida ya masomo ya aina mbalimbali.