Maua yamepangwa kwa umaridadi yakitoa harufu nzuri katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), harufu yake imechanganyika na harufu ya ikhlasi na uwajibikaji wa undugu wa Husseiniyya unao tokana na kubba hili tukufu, na unawaambia watu walio kuja kufanya ziara: Mwenyezi Mungu amekujalieni kua miongoni mwa wasubiriaji na mmefuzu kwa kumnusuru atakaye lipa kisasi chake (a.s), imamu Hujjat Mahadi (a.f).
Katika mazingira yaliyo jaa fufaha kutokana na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa walimwengu Swahibu Asri wa Zamaan Imamu Hujjat Almuntadhir (a.f), dirisha la Abulfadhil Abbasi (a.s) limepambwa kwa aina mbalimbali za maua, miongoni mwa aina hizo ni: Anturiam, Zanbaq, Waridi ya Holand, Kilayul, Rozi, Laalah, Kamilian, Joriy na Muhammadiy, haya ni maua ubora yana rangi yenye mvuto inayo ongeza furaha katika mnasaba huu mtukufu.