Utukufu wa ziara ya imamu Hussein (a.s) katika usiku wa nusu ya mwezi ya Shabani..

Maoni katika picha
Zimepokewa riwaya nyingi zinazo eleza utukufu wa kumzuru imamu Hussein (a.s) katika usiku huu mtukufu, hakika thawabu za ziyara ya imamu Hussein (a.s) sawa uwe mbali au karibu ni vigumu kuzielezea, imamu Hussein (a.s) ananyakati maalumu na mazingira rasmi ambayo yamesisitizwa kumzuru, miongoni mwa ziara maalumu ni hii ya mwezi kumi na tano Shabani, tutataja kwa ufupi shuhuda zinazo thibitisha utukufu wake:

  • 1- Kutoka kwa Abii Abdillahi anasema: (Katika usiku wa mwezi kumi na tano Shabani, atakaye kua katika aridhi ya Karbala, akasoma mara elfu moja (Qulhuwa llahu Ahad) na akaomba istigfari mara elfu moja , na akamhimidi mara elfu moja, kisha akasimama na kuswali rakaa nne, katika kila rakaa akasoma ayatu kursiyyu mara elfu moja, Mwenyezi Mungu humpa malaika wawili wanao mlinda katika kila jambo baya na wanamlinda na shetani, na wanamuandikia mema yake, wala haandikiwi maovu, na wanamuombea msamaha kwa muda wote atakao kua nao).
  • 2- Kutoka kwa Abii Hamza Shimaaliy anasema: Nilimsikia Ali bun Hussein (a.s) anasema: (Atakaetaka kupewa mkono na mitume laki moja na ishirini na nne elfu, amzuru imamu Hussein (a.s) katika usiku wa nusu ya mwezi wa Shabani, hakika malaika na roho za mitume huomba ruhusa kwa Mwenyezi Mungu ya kuja kumzuru (a.s) naye huwaruhusu, amefaulu atakaye peana mikono nao, miongoni mwao kuna mitumu watano ulul-azmi, ambao ni: Nabii Nuhu, Ibrahim, Mussa, Issa na Muhammad (s.a.w.w), nikauliza: kwa nini wameitwa Ulul-azmi? Akasema: (kwa sababu walitumwa mashariki na magharibi kwa majini na binadamu).
  • 3- Kutoka kwa Abii Abdillahi (a.s) anasema: (Inapo fika siku ya kwanza ya mwezi wa Shabani hutokea wito chini ya Arshi: Enyi wageni wa Hussein msiuache usiku wa nusu ya mwezi wa Shabani bila kumzuru Hussein (a.s) lau mngejua utukufu wake mngekaa mwaka mzima mkiisubiri siku hiyo).
  • 4- Kutoka kwa Yunusi bun Yaqoob anasema: alisema Abii Abdillahi (a.s) (Ewe Yunusi usiku wa nusu ya mwezi wa Shabani Mwenyezi Mungu humsamehe kila mwenye kumzuru Hussein (a.s) miongoni mwa waumini, na huambiwa: fanyeni ibada, akasema: nikasema: malipo yote hayo ni kwa atakaye mzuru Hussein (a.s) katika usiku wa nusu ya Shabani? Akasema: Ewe Yunusi lau watu wangeambiwa malipo anayo pata mwenye kumzuru Hussein (a.s) wangesimama watu wote hata kwa mbao!).
  • 5- Imepokewa kutoka kwa Abii Abdillahi Barqiy anasema: Abii Abdillahi (a.s) aliulizwa: Kitu gani anapata atakaye mzuru imamu Hussein (a.s) siku ya nusu ya mwezi wa Shabani kwa ajili ya kutafuta radhi ya Mwenyezi Mungu, akasema: (Mwenyezi Mungu humsamehe katika usiku huo dhambi zake hata kama zikiwa nyingi kama manyoya ya mbuzi). akasema: Ni kweli Mwenyezi Mungu humsamehe madhambi yote?! Akasema: (Unaona ni jambo kubwa hilo kwa mwenye kumzuru Hussein (a.s)? kwa nini asisamehewe wakati ana hadhi sawa na aliye mzuru Mwenyezi Mungu katika arshi yake!).
  • 6- Katika hadithi nyingine iliyo pokewa na imamu Swadiq (a.s) anasema: (Mwenyezi Mungu humsamehe mwenye kumzuru imamu Hussein (a.s) katika usiku wa nusu ya mwezi wa Shabani dhambi zote zilizo tangulia na zilizo chelewa –alizo fanya na ambazo hajafanya-).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: