Haikua siku ya kawaida.. wala sio tukio la kawaida.. hakika ni siku ya kuzaliwa muokozi wa wanadamu na mkombozi wa walimwengu usiku wa (14 Shabani 255h), baada ya kupita miaka (1380), katika siku ya (14 Shabani 1435h) kabla ya miaka mitatu, Marjaa dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Sistani (d.dh.w) alitoa fatwa ya kihistoria aliyo okoa Iraq na nchi za mashariki, fatwa ya wajibu kifaiyya (kutoshelezeana) wa kujilinda dhudi ya uadui wa kinyama uliokua unafanywa na magaidi ya Daesh, kwa ajili ya kuilinda Iraq na maeneo matukufu na kulinda roho za raia na heshma yao, na ikabainisha kua atakaye uawa katika kutekeleza hili atakua amekufa shahidi.
Kutokana na fatwa hii iliyo pata nguvu kwa mwitikio mkubwa wa raia walio itikia wito wa Marjiiyya mkuu wa kusimama pamoja na jeshi, mikoa yote ya Iraq ilishuhudia makundi ya watu wa aina zote wakitoka kuitikia wito huo.
Wananchi wa Iraqi wote waliitikia fatwa ya jihadi kifaiyya ya kujilinda na walitoka wazee kwa vijana kwa ajili ya kulinda nchi yao, jambo hilo linafaa kuandikwa kwa wino wa dhahabu, Hashdi Sha’abi (wapiganaji wa kujitolea) waliundwa na tabaka zote za wananchi wa Iraq, wakawa tekemeo kubwa kwa jeshi la Iraq na ngao imara dhidi ya magaidi, wakapigana kwa ujasiri mkubwa na wakajitolea muhanga kwa hali ya juu kabisa.
Kumbuka kua mara ya kwanza kabisa fatwa hii ilitangazwa katika ukumbi wa haram ya Abul-ahraar imamu Hussein (a.s), katika minbari ya swala ya Ijumaa kupitia sauti ya mwakilishi wa Marjaa dini mkuu Muheshimiwa Shekh Abdulmahadi Karbalaiy (d.i) ambaye alisema kua: (Hakika kuwalinda watu wetu kwa kushika siraha au kitu chochote cha kujihami ni jambo tukufu, limethibitika hilo baada ya kubaini kua; mwenendo wa hawa magaidi ni mwenendo wa kidhwalimu na uko mbali kabisha na mafundisho ya uislamu, hawataki kuishi na watu kwa amani, wanamwaga damu na kuchochea ubaguzi katika miji ya Iraq na nchi zingine, enyi ndugu zetu wanajeshi, mnatekeleza jukumu la kihistoria, kizalendo na kisheria, yafanyeni nia yenu ni kuilinda Iraq tukufu na kulinda umoja na amani kwa wananchi pamoja na maeneo matukufu yasibomolewe na muondoe shari iliyo ikumba nchi hii na watu wake.
Wakati huu ambao Marjaa dini mkuu anasisitiza kuwasaidia na kusimama pamoja na nyie, mnatakiwa kupambika kwa ushujaa, ujasiri na subira, atakaye fariki kwa ajili ya kuilinda nchi yake na raia wake atakua amekufa shahidi –inshallah- … tunaomba baba amuhimize mwanaye na mama pia amuhimize mwanaye hali kadhalika mke amuhimize mumewe kutoka na kwenda kupigana kwa ajili ya kulinda heshima ya nchi hii na raia wake).