Kufika kilele cha ziara ya Shaabaniyya: Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya kila iwezalo katika kuwahudumia mazuwaru..

Maoni katika picha
kufika kilele cha ziara ya Shaabaniyya tukufu wakati wa Isha-ain, yaliongezeka makundi ya mazuwaru kutoka kila sehemu wakija kumzuru imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), na kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa wanadamu na mfalme wa zama hizi imamu Hujjat Muntadhir (a.f), Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kila iwezalo katika kutoa huduma kwa mazuwaru watukufu, wanajitahidi kuwafikia mamilioni ya mazuwaru ili kuwarahisishia kutekeleza ziara zao kwa ufanisi.

Kila kitengo cha Atabatu tukufu kinatekeleza majukumu yake kama yalivyo pangwa, ukizingatia kua siku hizi kuna ongezeko la hali ya joto, ikiwa ni pamoja na kuweka mazingira rafiki yanayo endana na utekelezaji wa ziara katika hali zote.

Kumbuka kua ziara ya tarehe kumi na tano Shabani katika kumbukumbu ya kuzaliwa kwa imamu Mahadi (a.f) ni ya pili kwa ukubwa na kuhudhuriwa na mamilioni ya watu baada ya ziara ra Arbainiyya ya imamu Hussein (a.s) ambayo hufanyika tarehe (20) katika mwezi wa Safar.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: