Idara ya maji: Maelfu ya lita za maji ya baridi yagawiwa kwa mazuwaru na wenye vikundi (maukibu) za kutoa huduma..

Maoni katika picha
Kama kawaida yao katika kila ziara: Idara ya maji chini ya kitengo cha (RO) kutoa huduma katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamegawa maelfu ya lita za maji kwa mazuwaru wa nusu ya mwezi wa Shabani na kenye vikundi vya Husseiniyya vinavyo toa huduma kwa mazuwaru, ugawaji wa maji ulufanyika katika maeneo mbalimbuli kama ufuatavyo:

Kwanza: Ndani ya ukumbi wa haram tukufu, walichaguliwa watumishi waliopewa jukumu la kukagua madeli kila wakati na kuhakikisha yamejaa maji safi ya baridi kutoka katika kituo maalumu kilicho andaliwa kwa shughuli hiyo.

Pili: Nje ya ukumbi wa haram, waliandaliwa watu waliokua na jukumu la kujaza maji ya baridi kwenye madeli yaliyo wekwa nje ya haram na katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu pamoja na katika njia zinazo tumiwa na mazuwaru wengi.

Tatu: Kugawa maji katika vikundi vya kutoa huduma kwa kiasi wanacho hitaji kwa kutumia magari yaliyo chini ya idara hii. Hali kadhalika tuligawa juis kwa mazuwaru kama sehemu ya kushirikiana nao katika furaha ya mnasaba huu mtukufu.

Kumbuka kua idara hii ilikua imejiandaa kwa muda mrefu, na ilikua imesha weka utaratibu wake kutokana na mahitaji ya maji, maji hayo wanatoa katika kituo cha Atabatu Abbasiyya tukufu na kuyahifadhi katika kituo kidogo cha idara ya maji, hapo kuna mitambo maalimu ya kuyatia baridi, kisha yanasambazwa katika mahodhi na kuwekwa kwenye madeli yakiwa yabaridi, watumishi hufanya kazi muda wote ili kuhakikisha hakuna sehemu inayo kosa maji.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: