Kituo cha ayfa chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na udogo wa eneo lake lakini kinafanya kazi kubwa ya kutoa huduma kwa mazuwaru, hususan katika siku za ziara zenye watu wengi ikiwemo ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani, watumishi wake wamejipanga kutoa huduma bora kwa mazuwaru watukufu, kupitia wahudumu waliopo katika eneo la katikati ya haram mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) tukufu na katika maeneo mengine yenye watu wengi.
Kuna vipindi viwili vya kazi kwa watumishi pamoja na wale wakujitolea , ambavyo ni asubuhi na jioni, wanafanya kazi saa (24) kwa kushirikiana na idara ya afya ya mji wa Karbala wameandaa fifaa tiba na dawa nyingi kwa ajili ya kutekeleza swala hili.
Asilimia kubwa ya matatizo wanayo kutana nayo yapo ndani ya uwezo wao na wanaweza kuyatibu, wakikutana na tatizo kubwa basi humpeleka mgonjwa huyo katika hospitali za karibu kwa kutumia magari ya wagonjwa ya Atabatu Abdasiyya tukufu yaliyopo katika maeneo yanayo zunguka haram tukufu.
Tunapenda kusema kua idara ya afya ya mji wa Karbala kwa kushirikiana na Atabatu Abbasiyya tukufu wamejipanga kutoa huduma ya ayfa kwa mazuwaru watukufu.