Kiwanda cha barafu cha Atabatu Abbasiyya tukufu chagawa maelfu ya vipande vya barafu kwa vikundi vinavyo toa huduma kwa mazuwaru watukufu..

Maoni katika picha
Kutokana na kuongezeka kwa joto imepelekea uhitaji wa barafu kua mkubwa, kwa ajili ya watu wanaokuja kumtembelea imamu Husseni na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), kiwanda cha barafu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinatoa kiasi kikubwa cha barafu na kuwapa idara ya maji ambao wamepanga watumishi wao kila eneo kwa ajili ya kugawa maji ya marudi.

Ugawaji huo unafuata utaratibu ulio wekwa na idara ya maji, ambapo waliangalia wingi wa watu katika kila eneo na kuweka matenki ya maji katika maeneo yenye watu wengi, yamesambazwa maelfu ya matengi katika maeneo mbalimbali ndani ya kipindi cha ziara hii, pia kuna baadhi ya vikundi (mawaakibu) za watoa huduma huenda moja kwa moja katika kiwanda cha barafu na kuchukua barafu.

Kumbuka kua kiwanda cha barafu cha Atabatu Abbasiyya ni miongoni mwa miradi ya kutoa huduma, lengo lake kubwa ni kuhudumia watu wanao kuja kufanya ziara katika Ataba na wakazi wa mji wa Karabala mtukufu, ni kiwanda kamili cha uzalishaji wa barafu safi, kinatumia teknolojia ya kisasa yenye uwezo mkubwa, kiwanda kipo katika majengo ya (R.O) Siqaau-2- (magodauni ya Atabatu Abbasiyya tukufu) katika barabara ya Baabil – Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: