Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kufanikiwa kwa ratiba yake ya ulinzi na utumishi katika kipindi cha ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani, walirahisisha upatikanaji wa mahitaji yote muhimu kwa mwanadamu, wamefanikiwa katika sekta zote, ya utoaji wa huduma na ulinzi wa amani, kutokana na juhudi kubwa za watumishi pamoja na mawasiliano baina yao, halikuripotiwa tukio lolote la uvunjifu wa amani, au hali ya msukumano mkubwa pamoja na wingi wa watu na ongezeko la joto, katika siku nne za mwisho kulikua na ongezeko kubwa sana la watu, ikiwemo usiku wa Ijumaa ambao ndio kilele cha ziara hiyo, Ataba iliwapanga watumishi wake pamoja na wale wa kujitolea katika maeneo tofauti ndani ya haram tukufu kwa ajili ya kuweka mazingira mazuri na kuwawezesha watu wanao kuja kufanya ziara wafanye ibada zao katika mazingira mazuri na kwa utulivu.
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unatoa shukrani kwa walinzi wa amani (askari) wote pamoja na watumishi wa Atabatu Abbasiyya wote na vikundi vya Husseiniyya na watoa huduma kwa mazuwaru (watu wanaokuja kufanya ziara) bila kuwasahau wale walio jitolea kuhudumia mazuwaru kwa namna moja au nyingine, kutokana na juhudi zenu mmeondoa ugumu na uzito kwa mazuwaru watukufu.
Kumbuka kua ziara ya nusu ya mwezi wa Shabani ambayo ni sehemu ya kukumbuka kuzaliwa kwa imamu Mahdi (a.f) ni ya pili kwa ukubwa baada ya ziara ya arbainiyya ya imamu Hussein (a.s) ambayo hufanywa tarehe ishirini katika mwezi wa Safar.