Miongoni mwa muendelezo wa kutoa huduma za kibinadamu kwa raia wa Iraq, Hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chili ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa mujibu wa maelekezo ya kiongozi wake mkuu wa kisheria Sayyid Ahmad Swafi (d.i), wamepunguza gharama ya matibabu kwa familia za mashahidi walio andikishwa katika taasisi ya mashahidi wa Iraq, kama sehemu ya kuunga mkono juhudi zinazo fanywa na taasisi hiyo kwa familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi.
Kiongozi mkuu wa hosputali dokta Haidari Bahadeliy amesema kua: “Taasisi ya mashahidi wa Iraq ina asilimia kubwa ya familia za mashahidi tofauti wa Iraq, kuna walio uliwa na utawala ulio pita (Sadam), walio uawa katika matukio ya kigaidi yanayo ikumba nchi hii pamoja na mashahidi wengine wengi, kwa ajili ya kuwakirimu na kuwapunguzia ukali wa maisha, utawala wa hospitali kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ukizingatia kua ndio mlezi wa miradi ya kibinadamu, umeamua kupunguza gharama za matibabu ya aina zote hadi upasuaji kwa kiasi cha asilimia thelathini (30%)”.
Bahadeliy akafafanua kua: “Yeyote aliye sajiliwa na taasisi tajwa hapo juu aende hospitali akiwa na vielelezo vyake ili ainginzwe katika orodha maalumu na awezo kuhudumiwa kwa mujibu wa punguzo hilo”.
Kumbuka kua hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu ina program nyingi za misaada ya kibinadamu kwa wakazi wa ndani na nje ya mkoa wa Karabala, kama vile program ya (bima ya afya) na program ya (matibabu bila malipo), pamoja na kutoa tiba bule kwa majeruhi wa Hashdi Sha’abi, ikiwa ni pamoja na kutoa huduma za afya katika program za Scaut na kuweka hema za huduma ya afya katika vipindi vya ziara ya mamilioni ya watu, hali kadhalika kukifanyia matengenezo kifaa tiba cha matatizo ya moyo katika hospitali ya Hussein (a.s) iliyopo Karbala, baada ya kusimama kufanya kazi kwa miezi kadhaa, na mambo mengine mengi.