Mtandao wa Alkafeel wa kimataifa chini ya idara ya intanet katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamesoma dua na kufanya ziara maalumu za nusu ya mwezi wa Shabani kwa niaba ya watu walio jisajili katika mtandao wao uliopo katika lugha za (Kiarabu, Kiengereza, Kifarsi, Kituruki, Kiurdu, Kifaransa, Kiswahili na Kijerumani), idadi ya watu walio fanyiwa ziara na mtandao wa Alkafeel katika kipindi hiki cha nusu ya mwezi wa Shabani ni zaidi ya (4000) kutoka katika miji tofauti.
Usajili wa ziara hii tukufu ulifanywa kwa muda wa siku tano, ili kutoa fursa kwa watu wengi zaidi, watu walio jisajili asilimia kubwa wanatoka katika nchi zifuatazo: (Iraq, Iran, Lebanon, Pakistan, Urusi, Marekani, Uwengereza, India, Saudia, Swiden, Kanada, Kuwait, Malesia, Australia, Aljeria, Baharain, Misri, Ujerumani, Islandi, Namsa, Yunani, Holandi, Tunusia, Damarik, Narwiji, Qatar, Ubelgiji, Morocco, Afghanistan, Oman, Ekwado, Brazil, Ajentina, Uswisi, Naijeria, Gana, Yemen, Indonesia, Itali, Hispania, Ufaransa, Uturuki, Adharbaijani, Saipras, Finlandi, China, Ireland, Hong Kong, Japani, Imarati na Sudani).