Sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa wanadamu imamu Mahdi (a.f) idara ya watoto na makuzi chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu imetoa mtiririko maalumu wa visa kuhusu uhai wa maimamu maasumu (a.s) wote.
Mtiririko huo umekusanya machapisho kumi na nne, kuanzia kwa Msema kweli muaminifu (s.a.w.w) hadi kwa imamu Muhammad Mahdi (a.f), machapisho hayo yameandikwa kwa majina ya maimamu waongofu (a.s) na laqabu zao, yameandika mazuri katika historia za Ahlulbait (a.s), kila imamu ameelezewa katika toleo lake maalum.
Mradi huu (wa kutoa mtiririko wa visa nya maimamu -a.s-) unalenga kuwajulisha watoto viongozi watukufu wa umma wa kiislamu, wafahamu majina yao kamili sifa zao na baadhi ya mambo waliyo fanya katika uhai wao, kazi hii imefanywa kwa muda wa miezi saba kamili, katika kipindi hicho ziligawiwa kazi kwa kufuata muda na zote ziliisha ndani ya muda ulio pangwa.
Kumbuka kua idara ya watoto na makuzi inachapisha majarida mawili ambayo ni: Riyaahain, linalo husiana na mambo ya watoto na Haidarah, linalo husu makuzi, pamoja na machapisho ya visa na mashairi ya kidini katika mradi h