Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu washiriki katika hafla ya kongamano la Baqiyyatu Llah la kitamaduni katika Masjid Sahla..

Maoni katika picha
Ugeni wa Atabatu Abbasiyya tukufu ukiongozwa na naibu rais wa kitengo cha habari na utamaduni Sayyid Aqeel Abdulhussein Yaasiriy umehudhuria hafla ya kuhitimisha kongamano la Baqiyyatu Llah awamu ya kumi lililo fanywa na uongozi wa Masjid Sahla kama sehemu ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa wanadamu imamu Mahdi (a.f), kongamano lililo kua na vipengele vingi kuhusu mnasaba huo.

Hafla hiyo ilifanyika katika ukumbi mkuu wa msikiti huo na ilipata mahudhurio makubwa kutoka kwa watu mbalimbali wakiwemo viongozi wa kidini, kisiasa na kitamaduni, hali kadhalika rais wa wakfu shia Sayyid Alaa Mussawiy (d.i) alihudhuria hafla hiyo, pamoja na idadi kubwa ya viongozi wa Ataba na mazaru tukufu na wawakilishi wa ofisi za Maraajii watukufu na kundi kubwa la mazuwaru.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu halafu ukafuata ujumbe wa Masjid Sahla ulio wasilishwa na katibu mkuu wa Masjid hiyo dokta Mudhwar Sayyid Ali Khaan Almadaniy, kisha ukafuata ujumbe wa wakfu shia ulio wasilishwa na Sayyid Alaa Mussawiy ambaye alieomba kuja haraka kwa faraja (kudhihiri Imamu) na akatoa shukrani na pongezi kwa uongozi wa Masjid Sahla kwa kuandaa kongamano hili kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu za Ahlulbait (a.s), uongozi wa Masjid Sahla ulimpa midani ya kumshukuru muheshimiwa Sayyid Alaa Mussawiy kutokana na juhudi zake endelevu za kusaidia maeneo matukufu, hali kadhalika uongozi huo ulitoa zawadi kwa Ustadh Huquqi Salaam Khafaji kiongozi wa wakfu shia katika mji wa Najafu Ashrafu, hafla hii ilipambwa na ujumbe kutoka kwa watu mbalimbali pamoja na Qaswida na mashairi kuhusu mnasaba wa kongamano.

Mwishoni mwa kongamano ulifanyika uzinduzi wa maktaba kuu ya Masjid Sahla katika ukumbi wa bibi Narjis (a.s) uliopo jirani na msikiti mtukufu, maktaba hiyo imejaa maelfu ya vitabu vya fani mbalimbali, vilevile ilifunguliwa maktaba ya kimtandao (kielektronik) ambayo inazaidi ya vitabu laki moja vya fani zote.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: