Kufunguliwa milango ya ushiriki katika mradi wa Amiri wa wasomi wa kitaifa..

Maoni katika picha
Kituo cha kuandaa wasomi na mahafidh wa Qur’an chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya kimefungua mlango wa kujiandikisha kila anaye penda kushiriki katika mradi wa Amiri wa wasomi wa kitaifa katika msimu wa mwaka (2017m).

Wamebainisha kua kujiandikisha kutafanyika kwa njia ya mtandao au piga simu hii (07818404679) kwa maelezo zaidi, mwenye kupenda kushiriki atume vitu vifuatavyo:

 • 1- Majina yake matatu.
 • 2- Tarehe ya kuzaliwa (siku – mwezi – mwaka) umri wake usizidi miaka (17).
 • 3- Jina la mkoa atokako.
 • 4- Jina la wilaya na kitongoji.
 • 5- Namba ya msimamizi wake, ambaye atakua ndio mdhamini wake atakapo kubaliwa.
 • 6- Namba ya mwalimu aliye mfundisha, ambaye atakua mdhamini wa mwanafunzi wake iwapo atakubaliwa.
 • 7- Namba yake ya simu.
 • 8- Kiwango cha elimu yake.
 • 9- Jina la shule.
 • 10- Je anaiga msomi wa zamani mkubwa yeyote? Miongoni mwa wasomi wa Iraq na Misri? Kama ndio, ni nani?
 • 11- Anafahamu visomo vya aina ngapi?
 • 12- Je anafahamu hukumu za usomaji?
 • 13- Je amesha wahi kupata ushindi wa usomaji? (ataje jina la mashindano, mahala yalipo fanyika na alikua mshindi wa ngapi)
 • 14- Aina zipi za visoma anavyo penda? (mbali na kuvisoma)
 • 15- Picha yake ya hivi karibuni akiwa katika usomaji.

Kituo kimesisitiza kua watakao tuma taarifa zao na kuomba kushiriki kama ilivyo elekezwa hapo juu, watume na vipande viwili vya video zao, ziwe na majina yao matatu pamoja na majina mawili wa wasomi wakubwa anao wapenda, anatakuwa kuzingatia mambo yafuatayo:

 • 1- Anatakiwa abainishe yupi katika wasomaji wakubwa anaye mpenda na kuiga usomaji wake, aandike chaguo lake la kwanza na la pili, asiandike mtu anaye penda kumsikiliza tu bali aandike mtu anaye penda kumwiga, ambaye kisomo chake kinafanana na mtu huyo, akichagua vibaya inaweza kupelekea kumtoa katika washiriki.
 • 2- Azingatie matamsi sahihi ya Qur’an.
 • 3- Msomaji atakae tuma vipande vya video vya aina moja mara mbili hatakubaliwa.

Kumbuka kua mradi wa Amiri wa wasomaji, unalenga kuandaa vijana wenye umri mdogo katika usomaji wa Qur’an kwa kuwapa semina za muda mfupi na kuwafundisha vitu muhimu, na walengwa wakubwa ni wanafunzi wa shule za msingi na upili (sekondari) kutoka katika mikoa yote ya Iraq, na kutumia vizuri muda wao wa likizo, tunakusudia kuandaa kundi kubwa la wasomi wa Qur’an na kuhakikisha wanakua na kiwango kizuri, ambapo hua wanapata mafunzo kwa muda wa miezi miwili takriban katika hatua ya kwanza ya mradi huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: