Jana Juma Nne (18 Shabani 1438h) sawa na (15 May 2017m) shughuli za kongamano la amani la kitamaduni awamu ya tisa zilianza, linalo simamiwa na uongozi wa Imamu Swadiq (a.s) wa kitamaduni kwa kushirikiana na Ataba za Alawiyya, Husseiniyya, Kadhimiyya na Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo: (Njia ya kukutana na kuonana katika jamii ndio moyo wa maelewano) katika kongamano hili wameshiriki watafiti na wasomi wa kihauza na kisekula kutoka ndani na nje ya Iraq, kongamano hili litakalo dumu siku nne ni sehemu ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa imamu Mahdi (a.f).
Kongamano hili lilihudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya na makatibu wakuu wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) na jopo la viongozi wa Ataba, pamoja na pamoja na idadi kubwa na wadau muhimu wa kidini, kitamaduni na kidekula, kongamano lilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukafuata ujumbe kutoka kwa kamati ya usimamizi wa kongamano ulio wasilishwa na Shekh Aqeel Ali Zubaidiy, miongoni mwa aliyo sema ni: “Wakati ambao wapiganaji wetu wanaendelea kupata ushindi dhidi ya magaidi na kuendelea kujinasua kutoka katika makucha yao na wasaidizi wao, zinafanyika juhudi za kuharibu fikra na maadili ya jamii kwa kutumia mwanya huu ambao watu wanashughulika na vita pamoja na kusaidia wapiganaji na wakimbizi kutokana na maelekezo ya Marjaa dini mkuu.
Kutokana na ukweli huo tunakuta kua majukumu yamekua mengi nay a aina tofauti, miongoni mwa neema za Mwenyezi Mungu katika mji huu, hususan uongozi wa Imamu Swadiq (a.s) wa kitamaduni wasimamizi wakuu wa kongamano hili, ni kupata nafasi ya kuchangia swala hili, na fahari kubwa kwetu ni kupata nafasi ya kumtumikia Baqiyyatu Llah (a.f), Alhamdu lilaahi tumeendelea kupata neema hii ya kufanya makongamano haya hadi sasa hivi ni mwaka wa tisa mfululizo, kwa fadhila za Mwenyezi Mungu mtukufu na baraka za Marjaa dini mkuu na msaada wa Ataba tukufu, tunamuomba Mwenyezi Mungu aijalie nchi yetu amani na baraka”.
Kisha ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio