Kongamano la kitamaduni: Atabatu Abbasiyya tukufu yafanya kumbukumbu ya fatwa ya kujilinda..

Maoni katika picha
Chini ya kauli mbiu: (Fatwa ni msingi wa ushindi na miski ya shahada) alasiri ya Alkhamisi (21 Shabani 1438h) sawa na (18 May 2017m) lilianza kongamano la fatwa ya kujilinda tukufu awamu ya pili katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s) chini ya usimamizi wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa ajili ya kumbukumbu ya kutolewa kwa fatwa tukufu ya kujilinda na Marjaa dini mkuu na namna ilivyo pata muitikio mkubwa kutoka kwa raia wa Iraq.

Kongamano hili lilihudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu na jopo la viongozi, pamoja na kundi kubwa la watu muhimu katika dini tamaduni na wasomi wa kisekula wakiwemo wapiganaji wa Hashdi Sha’abi, ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, halafu ukaimbwa wimbo wa taifa ukafuatiwa na wimbo wa Ataba, kisha kiongozi wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahamad Swafi (d.i) akawasilisha ujumbe wake, miongoni mwa aliyo sema ni: “Mwitikio wa haraka wa fatwa ya kujilinda ulivunja malengo ya Daesh, fatwa tukufu na namna raia wa Iraq walivyo ipokea kwa haraka ilisimamisha na kuharibu kabisa malengo ya Daesh, mambo yakapangwa vizuri ushindi ukaanza kupatikana na tumeendelea kupata ushindi hadi hapa tulipo fika leo kwa uwezo wa Mwenyezi Mungu mtukufu..”.

Ikaimbwa Qaswida ya kimashairi iliyo burudisha masikio ya wahudhuriaji na mshairi maarufu Najaah Arsaan ambaye alisifu ushujaa mkubwa walio onyesha wananchi wa Iraq katika kuitikia fatwa tukufu ya kujilinda.

Halafu akazungumza kiongozi mkuuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji Ustadh Maitham Zaidiy, miongoni mwa aliyo sema ni: “Ni furaha kubwa na fahari ilioje kupata nafasi ya kuzungumza kwa niaba ya kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) katika hafla tukufu kama hii mbele ya Marjaiyya na wairaq, Marjaiyya walio hifadhi aibu ya wairaq kwa fatwa yake tukufu ambayo ilikua ni ponyo na liwazo kwa majeruhi, daima tunapo taja neno (Hashdul Qudsi) tunajiuliza sana kwa nini neno (Hashdi) limefungamana na neno tukufu la (Qudsi), tunafahamu kua Iraq kulikua na harakati nyingi katika ngazi ya idara na katika ngazi ya jeshi, kwa nini haikuitwa (Isnadul Muqadasi) au (Swahwatul Muqadasi?!!) pamoja na kwamba ilipata muitikio mkubwa sana katika ngazi ya idara”.

Akabainisha kua: “Hashdi wamepata utukufu kutokana na fatwa tukufu ya Marjaiyya iliyo tolewa katika mji wa Najafu Ashrafu ikaweza kulinda nchi yetu na dunia nzima kwa ujumla, kwa sababu adui huyu amekuja kubomoa ubinadamu, halengi dini peke yake au kundi fulani peke yake bali analenga kuvunja misingi ya ubinadamu, lakini fatwa ya Marjaiyya tukufu iliyo pokelewa kwa haraka na wairaq imeweza kuharibu njama zao”.

Akaendelea kusema kua: “Sisi kama raia wa Iraq tunajivunia nchi yetu kuhifadhi miili mitakasifu ya maimamu wa Ahlulbait (a.s) pia tunajifaharisha kua nchi hii ndio atakayo fariki imamu Hujjat msubiriwa (a.f) atakae jaza dunia haki na uadilifu kama ilivyo jaa dhulma na uovu, sisi kama wairaq tunaona ni utukufu kua walengwa wa kwanza wa kiongozi huyu mtukufu atakapo kuja kuikomboa dunia, na Mwenyezi Mungu kuiteua aridhi yetu kuhifadhi maimamu sita watakasifu (a.s) na kua ndio sehemu aliyo zaliwa imamu Hujjat Msubiriwa, na kuwajalia wairaq kua watekelezaji wa fatwa tukufu ya Marjaiyya, haya hayajafanyika bure, bali yameandaliwa, lau tungesimuliwa tungesema hizo habari za kale lakini tumejionea wenyewe na tumeishi katika mazingira hayo, na kisa hiki kitaendelea kuwepo watajifaharisha kwacha watoto na wajukuu wetu, sitaki kurefusha sana nitamalizia kwa maneno mawili kuhusu wananchi wa Iraq watukufu, hususan katika aridhi tukufu ya Najafu Ashrafu iliko tolewa fatwa..”.

Halafu ikaonyeshwa filamu iliyo tengenezwa na idara ya Alkafeel katika Ataba tujufu, inayo onyesha huduma zinazo tolewa na Marjaa dini mkuu kwa familia za wakimbizi kuanzia kaskazini hadi kusini ya Iraq, kisha ukatangazwa mradi wa kuandaa mtiririko (mausua) wa fatwa ya kujilinda tukufu unao gharamiwa na Markaz Ameed Duwaliy Lilbuhuthi wa Dirasaat iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Baada ya hapo wahudhuriaji wote wakaelekea katika uwanja wa katikati ya harama mbili tukufu kwa ajili ya uzinduzi wa maonyesho ya picha za mnato zinazo onyesha ushindi wanaopata wapiganaji watukufu watekelezaji wa fatwa ya kujilinda, palikua na picha nyingi zinazo onyesha matukio mbalimbali zilizo andaliwa na wataalamu wa nje na ndani ya Ataba tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: