Kamati ya maandalizi ya kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda mwaka wa pili linalo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatwa ni msingi wa ushindi na miski ya shahada) imetoa maelekezo maalumu, kupitia ujumbe ulio wasilishwa na mjumbe wa kamati hiyo na naibu rais wa kitengo cha habari na utamaduni Sayyid Aqeel Yasiriy katika hafla ya kuhitimisha kongamano hilo iliyo fanywa siku ya Alkhamisi (22 Shabani 1438h) sawa na (19 May 2017m), ifuatayo ni sehemu ya maelekezo hayo:
- 1- Umetolewa wito kwa waandishi watukufu; kuandika ushindi wa Hashdul Muqadas na jeshi letu tukufu, ili taarifa hizi zirithishwe katika vizazi vijavyo, kama walivyo anza Atabatu Abbasiyya tukufu kutoa mtiririko (mausua) ya fatwa tukufu ya kujilinda.
- 2- Kuhimiza pande zinazo shiriki katika kukomboa aridhi watunze kumbukumbu za tarehe walizo pata ushindi na vikosi vilivyo shiriki, jina la opresheni yao, idadi kamili na majina ya wapiganaji walio pata shahada katika opresheni hiyo, na kuzikabidhi kumbukumbu hizo katika makumbusho ya Atabatu Abbasiyya tukufu na katika maktaba na nyumba ya nakala kale (daru makhtutaat) ya Atabatu Abbasiyya pamoja na nyumba ya vielelezo vya kiiraq (daru wathaaiq al-iraaqiyyah), kwa ajili ya kutunza ushindi huu mtukufu ambao Marjaiyya mtukufu amehimiza mara nyingi kutunzwa kwa taarifa hizi kwa ajili ya vizazi vijavyo.
- 3- Kuhimiza vyombo vya habari vyote kwa ujumla kupanua wigo wa kutangaza ujasiri na ushujaa wa wapiganaji walio itikia wito wa fatwa tukufu ya kujilinda na kuandaa filamu.
- 4- Kuendelea kufanywa kongamano hili kila mwaka na kuonyesha nafasi ya Ataba tukufu katika kuifanyia kati fatwa na huduma za kibinadamu walizo toa.
- 5- Kujiepusha na kila jambo linalo weza kuleta fitna, chuki au kupunguza hisia za utaifa, tuwaachie watu walio bobea katika uandishi wafanye kazi yao (ya kuliunganisha taifa).
- 6- Umetolewa wito kwa wenye mamlaka kuweka siku maalumu za kuwakumbuka mashahidi wa fatwa tukufu ya kujilinda katika miji na vitongoji vyao, na kuendelea kuenzi mihanga yao, ili vizazi na vizazi viendelee kuwakumbuka kwa kukomboa nchi yao tukufu.