Atabatu Abbasiyya tukufu yahitimisha kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda na yaahidi kuendelea kufanya kila mwaka..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha habari na utamaduni alasiri ya Ijumaa (22 Shabani 1438h) sawa na (19 May 2017m) wamehitimisha kongamano la fatwa tukufu ya kujilinda katika mwaka wa pili chini ya kauli mbiu isemayo: (Fatwa ni msingi wa ushindi na miski ya shahada) lililo dumu siku mbili.

Hafla ilifanyika katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu, hafla hiyo ilipata mwitikio mkubwa kutoka kwa tabaka mbalimbali za jamii, ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu kisha ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq na ukasikilizwa wimbo wa taifa na ule wa Ataba tukufu huku watu wakiwa wamesimama.

Halafu ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu ulio wasilishwa na Shekh Kamaal Alkarbalaiy kutoka katika kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu, ambapo alisema kua: “Juhudi zetu katika jihadi ya kujilinda ni kuwalinda wanadamu wote bila kubagua, ili tuwabainishie walimwengu kua dini yetu ya kiislamu ni dini ya kibinadamu na amani na haikubali dhulma na uovu, raia wa nchi hii wana imani sahihi, nchi hii tukufu inamwaga damu kwa ajili ya kulinda heshma ya nchi na maeneo matukufu”.

Kisha baada yake ukafuata ujumbe wa kamati ya maadhalizi ulio wasilishwa na mjumbe wa kamati hiyo Sayyid Aqeel Abdulhussein Yasiriy, ambaye alisema kua: “Sisi ni umma ambao tumepokea vizuri wito wa Marjaiyya yetu tukufu na tumeitikia vizuri, kwa kua sisi ni umma tunao shuhudia magumu na machungu, hili limepelekea tujitolee kwa hali na mali katika kupambana na genge la magaidi la Daesh, Mwenyezi Mungu abariki juhudi hizi zinazo ilinda na kuihami aridhi ya mitume, maimamu na mawalii, aridhi ya watu wastarabu walio asisi kanuni ya kwanza ya ustarabu kwa walimwengu”.

Sayyid Aqeel akaendelea kufafanua vipengele muhimu katika kongamano na akasisitiza kua kongamano hili litafanywa kila mwaka na litaboreshwa zaidi, pamoja na kuelezea nafasi ya Ataba tukufu katika kuifanyia kazi fatwa hiyo tukufu na waliyo yafanya katika huduma za kibinadamu.

Kisha yakatangazwa majina ya washindi wa shindano la kongamano na wakapewa zawadi, ilikua kama ifuatavyo:

Kwanza: Washindi wa visa vifupi:

  • 1- Sihru Shami.
  • 2- Dhuha Ridhwa.
  • 3- Mustwafa Aadil.
  • 4- Swadiq Mahdi Hassan.
  • 5- Najaah Hussein.

Pili: Washindi wa Makala:

  • 1- Hussein Ali Hussein Sharifi.
  • 2- Adiy Mukhtaar.
  • 3- Hassan Ali Jawaad.
  • 4- Bushra Mahdi Budeirah.
  • 5- Jameel Maanii Bazuni.

Tatu: Washindi wa shindano la utafiti:

  • 1- Mtafiti raia wa Lebanon Yusufu Bayumi Ridhwawiy.
  • 2- Khadija Hassan Qaiswar.
  • 3- Dokta Muhammad Jameel Auda Almayahiy.
  • 4- Ustadh Luaiy Abdurazaaq Farju-Llah.

Kutokana na umuhimu na kuonyesha thamani ya misaada inayo tolewa na vikundi vya Husseiniyya kwa wapiganaji wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi nao pia wakapewa zawadi, na mwisho kabisa zikatolewa zawadi kwa vyombo vya habari vyote vilivyo tangaza matukio ya kongamano hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: