Hospitali ya rufaa Alkafeel yahuisha siki ya kimataifa ya daktari wa familia..

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imehuisha siku ya kimataifa ya daktari wa familia, kwa kusimamia nadwa ya kielimu iliyo endeshwa na jumuia ya waganga wa familia wa kiiraq, ambayo iliangazia nafasi ya madaktari wa familia katika kutoa malezi ya kiafya, pamoja na kujikita zaidi katika kujadili maradhi ya Unyogofu na sababu ya kupatikana kwake na namna ya kuyatibu.

Nadwa ilifanyika katika ukumbi mkuu wa haspitali na ilipata muitikio mkubwa kutoka kwa madaktari, walimu wa vyuo na viongozi wa taasisi za afya kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala pamoja na mjumbe wa kamati ya afya ya bunge Muheshimiwa Dokta Swaaleh Hasanawiy.

Rais wa jumuia ya madaktari wa familia wa kiiraq Dokta Lajiin Khazrajiy alisema kua: “Nadwa yetu ya kielimu inafanyika siku ya kimataifa ya daktari wa familia na imependekezwa kujadili maradhi ya Unyogofu, maprofesa na madaktari wameelezea sababu za maradhi hayo na namna ya kuyagundua na kuyatibu, ukizingatia kua maradhi haya yameanza kuathiri wananchi wa Iraq, hadi sasa watu wengi sana wameathirika na maradhi haya, kwa mujibu wa utafiti ulio fanywa na kituo cha afya mjini Bagdad, asilimia sabini ya watu walio fanyiwa utafiti walikua wameathirika na maradhi hayo kwa namna moja au nyingine, pia utafiti huo ulibaini kua wairaq wana uwezo mkubwa wa kuvumilia matatizo yaliyo ikumba nchi yao kwa miaka mingi”.

Akamalizia kwa kusema: “Tunashukuru sana hospitali ya rufaa Alkafeel kwa kua wenyeji wa nadwa hii ambayo tunatarajia ilete matokeo chanya katika utendaji, pia tunatarajia kuendelea kufanya nadwa na warsha zingine zitakazo jadili aina nyingine za maradhi yanayo husu madaktari wa familia”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: