Inafanya kazi kimya kimya wakiwa mbali na vyombo vya habari, kamati ya misaada chini ya ofisi ya Muheshimiwa Sayyid Sistani (d.dh) kutokana na maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwake wanaendelea kuzisaidia familia za watu wanao kimbia mateso ya Daesh katika miji ambayo inashuhudia vita kali vinavyo endeshwa na jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi dhidi ya magaidi ya Daesh, kamati hii ambayo haijawahi kuacha kutoa misaada pamoja na hali ya hewa ngumu na mazingira hatari bado wanafanya kazi kimya kimya.
Kamati inafanya kazi kwa kushirikiana na taasisi ya Ain, hivi karibuni wamefanya msafara wa kwenda kutoa misaada kwa watu wanaokimbia vita upande wa kulia wa mji wa Mosul, katika mahema ya wakimbizi yaliopo kitongoji cha Jud’ah namba tano kusini ya Qayarah, ambayo yana idadi kubwa ya wakimbizi, walipewa vikapu (2500) vya nafaka pamoja na maziwa ya watoto na misaada mingine.
Kumbuka kua msaada huu ni sehemu ya misaada mingi inayo tolewa na ofisi ya Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani (d.dh) katika miji mbalimbali yaliko tokea mapambano ya kukomboa miji iliyo kua imetekwa na magaidi ya Daesh, kamati hii ilikua ni ya kwanza kutoa misaada ya lazima kwa familia za wakimbizi walio pata mateso ya Daesh.
Familia hizo zinaishi katika mazingira magumu sana kutokana na kuongezeka kwa joto, na kukosekana sehemu muafaka kwa kuishi, kwani wamekusanywa sehemu za dharura ambazo hazikua rasmi kwa ajili ya maisha, kumbuka kua idadi ya wakimbizi inaongezeka kila siku, inahitajika kuongeza juhudi zaidi.