Mfuasi wa Ahlulbait (a.s) na mpenzi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) atoa zawadi ya mswala wa thamani katika malalo yake takatifu..

Maoni katika picha
Kuonyesha ukubwa wa mapenzi yake kwa Abulfadhil Abbasi (a.s) yasiyo linganishwa na kiu chochote, mmoja wa wafuasi wa Ahlulbai (a.s) kutoka Iran katika mji wa Isfahan bwana Ali Hakimiy ametoa zawadi ya thamani zaidi ambayo ni mswala wa kutengenezwa kwa mikono, alikua na ndoto za kupata utukufu wa kuandikwa jina lake katika orodha ya watu waliotoa zawadi katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kutokana na maelezo yake bwana Ali Hakimiy; kazi ya kutengeneza mswala huu imechukua miaka mitatu hadi kuonekana katika uzuri huu, jambo kubwa alilo kua akitaka katika nafsi yake ni mswala huo utandikwe katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ilia pate kutabaruku kwa nyao za mazuwaru.

Kutokana na furaha za wafuasi wa Ahlulbait (a.s) katika mwezi wa Shabani, kitengo cha ulezi wa haram tukufu katika Atabatu Abbasiyya kiliutandika mswala huo katika mlango wa Qibla (babul qibla) wa haram hii tukufu, kwa mujibu wa bwana Ali Hakimiy mswala huo umetengenezwa kwa nyuzi za kienyeji na hariri halisi, nao ni miongoni mwa aina bora zaidi na rangi zake hazichuji, umetengenezwa kwa mikono kwa kutumia mapambo ya kienyeji na mimea, una muonekano mzuru unao endana na miswala ya haram tukufu.

Ukubwa wa mswala huo ni (mt4 x 7) una rangi nzuri ambazo ndio zinawekwa kwa mara ya kwanza katika haram hii tukufu, una rangi ya kijani iliyo tiwa rangi ya njano na nyeupe.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha pokea vitu mbalimbali kutoka kwa wafuasi wa Ahlulbait (a.s) wa ndani na nje ya Iraq amabao hutoa kama nadhiri au zawadi, vitu hivyo hupokelewa kwa utaratibu maalumu ambapo huandikwa nakala mbili, moja hupewa mtoaji na nyingine hutunzwa katika daftari maalumu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: