Mafundi wa maraya wanaendelea na kazi yao ya kukarabati maraya za haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
Mafundi wa maraya chini ya kitengo cha usimamizi wa kihandisi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wanaendelea na ukarabati wa maraya za haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kuondoa zilizo haribika na kuweka mpya, hadi sasa wamesha kamilisha upande wa minara na sehemu ya upinde katika mlango wa Mussa Kadhim (a.s) na kazi inaendelea katika upande wa mlango wa Swahibu Zamaan (a.f) na upande wa mlango wa kichwa kitukufu.

Kwa maelezo zaidi kuhusu matengenezo haya mtandao wa Alkafeel uliongea na kiongozi wa idara ya maraya Ustadh Hassan Said ambae alisema kua: “Hadi sasa tumesha kamilisha matengenezo upande wa mlango wa imamu Mussa Kadhim (a.s) na sehemu ya kuta maalum za haram tukufu, pamoja na kuweka marumaru na kurejeshea maraya sehemu ya minara na kazi inaendelea upande wa mlango wa Swahibu Zamaan (a.f) na sehemu ya mlango wa kichwa kitukufu, katika matengenezo haya mafundi walikutana na vikwazo vingi, kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu na baraka za mwenye malalo haya pamoja na jitihada za mafundi wetu waliweza kukamilisha kazi kwa ufanisi mkubwa”.

Akaongeza kusema kua: “Kazi ilikua na hatua nyingi, kwanza ilikua kuondoa maraya za zamani zilizo haribika na kuonekana waziwazi athari ya uharibifu wake, hii ilitokana na kukaa muda mrefu bila kubadilishwa, mafundi wetu walizitoa kwa kutumia kifaa cha kisasa kijulikanacho kama (Alatycaruat) kifaa ambacho hutumika kwa kutindulia kuta zilizo haribika na kupasuka pasuka, kifaa hicho husaidia kuzirekebisha, baada ya kuzitindua inafuata hatua ya kuziwekea aina ya vyuma vya (BRC) pamaja na vifaa vingine”.

Akafafanua kua: “Kisha inafuata hatua ya kuweka vifaa vya mbao (Plaud) hutumika kwa ajili ya kushikilia kuta, baada ya kumaliza hatua hiyo huwekwa (Selkon) kama ilivyo kua zamani lakini kwa kufanyiwa baadhi ya maboresho kisha ukuta hupakwa chokaa maalumu yenye ubora wa hali ya juu, kisha hufuatia hatua ya kuweka maraya zilizo tengenezwa kwa umaridadi mkubwa”.

Tunapenda kukumbusha kua idara ya maraya inaendelea na kazi ya kutengeneza na kukarabati maraya katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa kubadilisha maraya zilizo haribika na kuweka mpya zenye rangi nzuri ya kuvutia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: