Kwa kuhudhuria kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu, kitengo cha habari na utamaduni siku ya Juma Nne (26 Shabani 1438h) sawa na 23 May 2017m) wamefanya hafla ya kimashairi kwa ajili ya mnasaba wa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Ammi wa Mtume na mzazi wa Amirulmu-uminina Sayyid Bat-haau Abuutwalib (a.s), katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Hafla ilikua na mahudhurio makubwa ya viongozi wa Ataba na watumishi wake pamoja na wageni mbalimbali, ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu ikafuatiwa na wimbo wa taifa na wimbo wa Atabatu Abbasiyya, halafu kiongozi wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Sayyid Ahmad Swafi akaongea, miongoni mwa aliyo sema ni: “Kwa masikitiko makubwa historia yetu ya kiislamu kwa miongo mingi haikua fea (haikutenda haki), imepotosha mambo mengi, kwa sababu waandishi wa historia hawakua huru, walikua wakijaribu kusema ukweli wanapewa mateso na misukosuko mingi, jambo hilo likasababisha kubadilisha ukweli wa mambo mengi katika historia..”.
Baada yake likafuata shairi lililo somwa na Mudhar Aalusiy kutoka Bagdad, shairi lake lilizungumzia utukufu wa Abuutwalib (a.s) na nafasi yake katika kumuhami Mtume (s.a.w.w), kisha akafuatia mshairi Najahu Arsaan kutoka Karbala, naye shairi lake lilianzia alipo ishia Aalusiy katika kumsifu Abuutwalib (a.s) na kusifu msimamo wake, halafu ikafuatia Qaswida yenye mashairi shirikishi iliyo ongozwa na Muhammad Aajibiy na kuitikiwa na wahudhuriaji wote, mlango wa Qaswida na mashairi ukafungwa na Nadhir Mudhafar kutoka Nnajafu, hafla ikahitimishwa kwa kugawa zawadi na vyeti vya ushiriki kwa washairi walio shiriki.