Kutokana na ubora mkubwa: Darul Kafeel yachapisha zaidi ya nakala milioni mbili za vitabu vya kufundishia vya wizara ya malezi ya Iraq na yakamilisha awamu ya kwanza ya kazi yake..

Maoni katika picha
Darul Kafeel ya uchapaji na usambazaji wa vitabu iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu imekabidhi kazi ya awamu ya kwanza ya vitabu vya masomo kwa wizara ya malezi ya Iraq, kwa mujibu wa mkataba ulio sainiwa na pande mbili wa kuchapisha nakala (2,685,000) za masomo ya ngazi zote kwa muhula ujao wa (2017- 2018), kituo hiki cha uchapishaji ndio pekee kilicho kamilisha kazi wizarani ndani ya muda ulio pangwa bila kuchelewa, na kwa ubora mkubwa kuanzia jarada hadi karatasi zake na rangi pamoja na vitu vingine.

Mkuu wa kituo cha uchapishaji Ustadh Farasi Ibrahim alisema kua: “Hakika kituo kinamiliki mitambo ya uchapishaji ya kisasa na inaendeshwa na watalamu wakubwa, ni mitambo ya kimataifa na inazidi ubora mitambo ya hapa nchini, miongoni mwa sababu muhimu zilizo ifanya wizara ya malezi kuipa kazi ya uchapishaji wa vitabu vyake Darul Kafeel ni kutokana na ufanisi wake katika uchapaji wa vitabu unao vutia wateja wa aina zote taasisi na watu binafsi, hakika machapisho yake yote yanaubora wa kimataifa na yamepasishwa na taasisi ya viwango ya Iraq”.

Akaendelea kubainisha kua: “Katika uchapishaji wa vitabu hivi tumezingatia mambo mengi, miongoni mwake ni:

  • 1- Aina ya karatasi, tumetumia karatasi kutoka Marekani nazo ni nzuri kwa mazingira na zina shikika vizuri.
  • 2- Rangi tulizo tumia zina mvuto mkubwa na muonekano mzuri zimeenda sambamba na maelekezo tuliyo pewa.
  • 3- Majarada ya vitabu yamewekwa vizuri, yanamuwezesha mwanafunzi kufungua kurasa za kitabu kwa urahisi na yanadumu kwa muda mrefu.
  • 4- Hati iliyo tumika ni nzuri, hii ni kutokana na ubora wa mitambo tuliyo nayo pamoja na wataalamu wetu.
  • 5- Namna ya ukusanyaji wa kurasa za kitabu na idadi ya kurasa.
  • 6- Wino uliotumika unaubora wa kimataifa na unaendana na aina ya karatasi pia ni rafiki wa mazingira.
  • 7- Ni kituo cha kiiraq na watumishi wake wote ni wairaq tunaiwezesha nchi kujitegemea na kuto tegemea vituo vya uchapishaji vya nje ya nchi.
  • 8- Kuwezesha uzalishaji wa ndani.

Kumbuka kua kuanzishwa kwa mradi wa Darul Kafeel ya uchapishaji na usambazaji wa vitabu ni miongoni mwa mikakati ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kujenga uwezo wa kujitegemea, na kuhakikisha tunamiliki mitambo itakayo tuwezesha kuchapisha vitabu, majarida na magazeti, aidha kuchangia katika kusambaza vitabu na majarida yenye ubora mkubwa na kwa gharama ndogo, kituo hiki kina mitambo bora na ya kisasa kabisa, kwa ajili ya kuondoa tatizo la mahitaji ya machapisho kwa Atabatu Abbasiyya na taasisi zingine.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: