Atabatu Abbasiyya tukufu yatangaza maandalizi ya kuupokea mwezi wa Ramadhani na yaandaa ratiba maalumu ya mwezi huo..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya imetangaza kukamilika kwa maandalizi ya kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani, ulinzi umeimarishwa na wamejipanga kutoa huduma kwa watu wanaokuja kumzuru Abuu Abdillahi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) ili kuwawezesha kufanya ibada na ziara kwa wepesi, tunalipa umuhimu mkubwa swala la kutoa huduma bora kwa mazuwaru watukufu wanao kuja katika aridhi hii tukufu ya Karbala kwa ajili ya kufanya ibada zao, kwa kua malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) ni sehemu ya pili inayo kusudiwa na watu baada ya kumzuru ndugu yake Abuu Abdillahi Hussein (a.s) basi tumeifanya kua mlango wa utukufu na utoaji, Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalumu ya mwezi huu na haya ni baadhi ya mambo yaliyopo katika ratiba hiyo:

 • 1- Kisomo cha Qur’an kwa watumishi wa Ataba na mazuwaru ndani ya ukumbi wa haram tukufu kila siku baada ya Dhuhurain.
 • 2- Kisomo cha Qur’an kitakacho shiriki wasomi maalumu kila siku Alasiri jioni watasoma juzu kamili.
 • 3- Kusoma dua ya Iftitaah kila siku na dua ya tawassul kila usiku wa Juma Tano na Kumail kila usiku wa Ijumaa.
 • 4- Kila siku kutakua na Muhadhara utakao tolewa na Shekh Twaaiy atazungumzia mambo tofauti pamoja na hukumu za funga.
 • 5- Kushiriki na kusaidia kufanyika kwa kongamano la imamu Hassan Almujtaba (a.s) kuhusu kuzaliwa kwake ambalo hufanywa kila mwaka, mwaka huu ikiwa ni awamu ya kumi katika mji wa Hillah.
 • 6- Kuendesha ratiba maalumu kuhusu kuzaliwa kwa imamu Hassan Almujtaba (a.s).
 • 7- Kutoa machapisho yanayo husu ubora na utukufu wa mwezi wa Ramadhani kila wiki au kila mwezi.
 • 8- Kuendesha ratiba maalumu ya kuomboleza kuanzia siku aliyo jeruhiwa imamu Ali (a.s) hadi siku aliyo fariki.
 • 9- Kuendesha ratiba maalumu ya kuhuisha siku za Lailatul Qadri.
 • 10- Kufanya mashindano ya Qur’an ya vikundi kila siku ndani ya huu mwezi mtukufu.
 • 11- Kuandaa vipindi maalumu kuhusu mwezi wa Ramadhani vitakavyo rushwa kila siku katika Idahaatul Kafeel ya wanawake.
 • 12- Kitengo cha dini kitatoa mihadhara kila siku na kujibu maswali pamoja na kufafanua hukumu za funga kwa mazuwaru na mengineyo.
 • 13- Kurusha program zote za Ataba kupitia masafa maalumu.

Hii ni sehemu ya mambo yatakayo fanywa na Ataba tukufu katika mwezi huu ambayo tumependa kuyabainisha kwenu, tuna muomba Mwenyezi Mungu mtukufu kupitia huduma hizo atupe shufaa ya Mtume (s.a.w.w), ubora ulioje wa kutoa huduma katika mwezi huu, ubora ulioje wa kufanya ibada katika mwezi huu, hususan yanapo fanyika hayo ndani ya nyumba alizo ruhusu Mwenyezi Mungu ziinuliwe (zijengwe) na litajwe jina lake ndani ya nyumba hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: