Ofisi ya Marjaa dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani (d.dh) inategemea kuonekana mwezi wa Ramadhani mtukufu jioni ya siku ya Ijumaa (29 Shabani 1438h) sawa na (26 May 2017m) katika anga la mji wa Najafu Ashrafu wakati wa kuzama jua saa (07:00) jioni na utaendelea kuonekana kaada ya jua kuzama kwa muda wa dakika (38), kiwango cha muonekano wake kitakua (%1,27) hivyo inatarajiwa utaonekana kwa shida pamoja na anga kua safi.
Taarifa hii imetolewa katika jaduali la kuandama kwa mwezi wa Ramadhani mtukufu mwaka (1438h) sawa na (2017m) iliyo tolewa katika mtandao wa Marjaa dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani (d.dh) katika mji wa Najafu Ashrafu.