Hospitali ya rufaa Alkafeel yapokea jopo la madaktari bingwa wa magonjwa mbalimbali kutoka Urusi na yasisitiza kua itaendelea kuwapokea zaidi..

Maoni katika picha
Hospitali ya rufaa Alkafeel iliyo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu iliwekeana mkataba na Urusi nyeupe unao husu kupokea madaktari kutoka Urusi na kuja kufanya kazi za kitabibu na upasuaji wa aina mbalimbali, kwa mujibu wa kiongozi wa hospitali dokta Haidari Bahadeli ambaye amesisitiza pia kua ataunda jopo lingine la madaktari wa kiiraq na watafanya kazi kwa kufuata kanuni na vigezo vya ulaya.

Akabainisha kua: “Baada ya jopo la madaktari wa Urusi kutembea hospitali kwa ajili ya kukagua vifaa tiba na uwezo ulionao hospitali ya rufaa Alkafeel, walionyesha kuvutiwa na wakataka tufungue milango ya ushirikiano baina yetu, makubaliano hayo yakawa ni tunda la kwanza la ziara yao, ndipo ukaandaliwa msafara rasmi ukiongozwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Muhammad Ashiqar (d.t) na wataalamu wa afya kutoka katika Atabatu Abbasiyya na hospitali ya rufaa Alkafeel na kuelekea katika nchi ya Urusi nyeupe kufuatia mwaliko rasmi kutoka huko”.

Akaendelea kusema kua: “Ugeni huo ulikutana na viongozi wa juu wa serikali ya Belarusia, akiwemo waziri mkuu, waziri wa afya na waziri wa viwanda, wakaingia mikataba ya ushirikiano katika sekta ya tiba na viwanda vya kutengeneza dawa, ndio ukatiwa saini mkataba wa kutuma madaktari bingwa wa maradhi mbalimbali na kuja kufanya kazi katika hospitali ya rufaa Alkafeel moja kwa moja na sio kuja kama ziara (kutembea) wanatarajiwa kuanza kazi hivi karibuni”.

Akasema kua: “Siku za mbele tutakua na makubaliano ya kufanya kazi kwa kushirikiana yanayo lenga kuhakikisha tunatoa huduma bora kabisa za kitabibu na yataturuhusu kuwapeleka madaktari wa kigeni katika hospitali zingine pia hapa Iraq”.

Kumbuka kua msafara ulioenda Urusi ulitembelea hospitali nyingi na ukakagua vifaa tiba vingi ikiwa ni pamoja na kutembelea kiwanda cha kutengeneza dawa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: