Kwa kushiriki makundi (24): Imeanza awamu ya tatu ya mashindano ya Qur’an tukufu..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi wa Ramadhani jioni ya siku ya Ijumaa (29 Shabani 1438h) sawa na (26 May 2017m) ilianza awamu ya tatu ya mashindano ya Qur’an ya vikundi yanayo simamiwa na kituo cha kuandaa wasomi na mahafidh wa Qur’an katika Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwa kushiriki makundi (24) kutoka katika miji tofauti ya Iraq, kila kikundi kinaundwa na watu watatu, (msomaji, hafidh na mfasiri) kutokana na utaratibu wa mashindano, mashindano yalifunguliwa na kikundi cha mji wa Muthannah na Diyala, mashindano haya yatadumu siku (15) kila siku yatashiriki makundi manne, washiriki wataulizwa maswali tofauti tofauti.

Maswali yanayo ulizwa yapo ya aina tofauti, kuna maswali ambayo yanapatikana baada ya kupigiwa kura, ambayo yanamtaka msomaji asome kwa namna fulani na msomaji analazimika kusoma kama ilivyo elekezwa, au inafunguliwa rekodi ya mmoja wa wasomaji wa zamani wa kimisri halafu anatakiwa ataje jina la msomi huyo, upande wa maswali ya hifdhu, anaweza kuambiwa kamilisha aya fulani au hafidh wa kwanza anasoma sehemu halafu hafidh wa pili anaendelea mbele ya alipo ishia hafidh wa kwanza, hii inaitwa kufukuzana (mutwarada) katika hifdh, na upande wa tafsiri anatajiwa aya anaifasiri na kuelezea hukumu za kisheria zinazo patikana katika aya hiyo au aya hizo.

Kuna jumla ya majaji wanne wanao angalia hukumu za usomaji wa Qur’an, saut na naghma, pia wanaangalia tafsiri, mada, kuanza na kusimama pamoja na hifdhu, msimamizi mkuu wa mashindano haya ni Sayyid Hasanain Halo, na yataisha usiku wa mwezi kumi na tano Ramadhani, ambayo ni tarehe ya kuzaliwa kwa imamu Hassan Almujtaba (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: