Shule za Ameed za pasisha na mmoja wa wanafunzi wake ashika nafasi ya kwanza katika mkoa wa Karbala..

Maoni katika picha
Kutokana na juhudi kubwa zinazo fanywa na shule za Ameed zilizo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu katika Atabatu Abbasiyya tukufu zimepata ufaulu wa (%100) kwa shule za mkoa wa Karbala katika mwaka wa masomo (2016/2017), kwa shule za msingi ambazo matokeo yake yametangazwa leo (28/05/2017m), kufaulu huku kunatokana na utaratibu mzuri ulio wekwa na uongozi wa shule pamoja na juhudi kubwa zinazo fanywa na walimu wetu watukufu.

Shule za msingi za Ameed zote mbili ya wavulana na wasichana zimefaulisha kwa (%100), shule ya msingi ya wavulana Sayyid Almaau imefaulisha kwa (%93) na mwanafunzi (Mina Haidari Nuriy Aboud) kutoka katika shule ya msingi ya Ameed ya wasichana ameshika nafasi ya kwanza katika mkoa wa Karbala kwa kufauli masomo yote kwa (%100), wanafunzi (51) wa shule hiyo wameshinda kwa zaidi ya (%90), huku wanafunzi (35) wa shule ya wavulana wakishinda kwa zaidi ya asilimia hizo pia.

Kumbuka kua kufaulisha kwa shule za Ameed kunatokana na ubora wa walimu wake na vitendea kazi vya kisasa walivyo navyo, ndio maana wamepasisha sana kushinda shule zote za mkoa mtukufu wa Karbala.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: