Ofisi ya Muheshimiwa Sayyid Sistani (d.dh) imebainisha hukuhu ya funga za wanajeshi wa serikali na wale wa kujitolea wanao endesha vita kali dhidi ya magaidi ya Daesh, hilo limepatikana katika jibu lililo tolewa na ofisi hiyo kutokana na swali lililo ulizwa na mmoja wa wapiganaji, mtandao wa kimataifa wa Alkafeel unakuletea swali hilo na jibu lake:
Muheshimiwa Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani (d.b)
Asalamu alaikum wa rahmatu llahi wa barakatuhu.
Nini hukumu ya funga ya ndugu zetu mujahidina wanao jitolea na wanajeshi wa serikali, wanao pitiwa na mwezi wa Ramadhani katika mazingira magumu ya joto kali huku wakilazimika kutekeleza majukumu waliyo pangiwa ya kivita?
Amani iwe kwenu na kwa waja wema wa Mwenyezi Mungu na rehema na baraka zake..
Jibu lilikua kama ifuatavyo:
Kwa jina la Mwenyezi Mungu mtukufu:
“Kilicho tajwa hakizuii kuweka nia ya funga wakati wa kuchomoza kwa Alfajiri, lazima unuie, lakini atakaye ona kua kuendelea kujizuia kula na kunywa kunamdhofisha katika kutekeleza wajibu wa lazima alio pangiwa, itajuzu kula na kunywa kwa kiwango cha lazima (Ihtiyaatu) na lazima ailipe siku hiyo.. mdum katika taufiq.
Ofisi ya Sayyid Sistani (d.dh) kitengo cha kutoa fatwa.