Idara ya harakati kuhusu Qur’an iliyo chini ya ofisi ya mahusiano ya vyuo vikuu katika Atabatu Abbasiyya tukufu imekamilisha nadwa yake kuhusu Qur’an iliyo kua miongoni mwa mradi ya kijana wa Alkafeel, ulio dumu mwaka huu wote wa masomo na kushirikisha idadi kubwa ya wanafunzi wa vyuo na maahadi za Iraq kwa kuwasiliana na wakuu wa vyuo na kufuata ratiba maalumu iliyo andaliwa bila kuathiri ratiba zao za masomo.
Ustadh Amru Alaa mkuu wa harakati kuhusu Qur’an aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Idara ya harakati kuhusu Qur’an ina mambo mengi yanayo husu Qur’an tukufu, inaendesha semina, warsha na nadwa kuhusu Qur’an, yote hayo yanalenga kujenga uelewa juu Qur’an na sheria zake kwa wanafunzi wa vyuo ili waweze kuishi kwa kufuata mafundisho ya Qur’an katika familia zao na jamii kwa ujumla”.
Akaongeza kusema kua: “Katika nadwa hizi, kuna kamati ambayo huchagua mashekh na huteuliwa mada maalumu ambayo hupewa shekhe aliye chaguliwa, naye hutakiwa kuiwasilishwa mada hiyo kwa undani huku akitumia aya na hadithi za maimamu wa Ahlulbait (a.s), baada ya kuwasilisha mada yake, hufunguliwa mlango wa majadiliano baina ya wanafunzi na hapo hutolewa nafasi ya kumuuliza maswali shekh aliye wasilisha mada, ambapo huulizwa maswali ya moja kwa moja au kwa kuandika katika karatasi, naye hutakiwa kujibu swali moja baada ya lingine”.
Akamalizia kwa kusema kua: “Kutokana na mafanikio makubwa tuliyo yaono, namna muitikio wa wanafunzi ulivyo kua mzuri, tutajitahidi kupanua mradi huu katika miaka ijayo na kuuboresha zaidi kwa kuongeza baadhi ya vipengele”.