Idara ya watalamu wa Alkafeel inayo husika na matangazo ya moja kwa moja chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza kukamilika kwa matengenezo ya masafa maalumu itakayo rusha bure matukio yote ya ratiba za mwezi wa Ramadhani pamoja na mambo mengine.
Wametoa wito kwa vyombo vyote vya habari (tv) za kitaifa na kimataifa zitakavyo penda kurusha matangazo hayo watayapata kupitia:
EUTELSAT 3B
Down 11,501.401 H
SR 2.966
Fes 3/4
Dvbs2-HD
Ratiba ya matangazo itakua kama ifuatavyo:
Kwanza: Qur’an tukufu kuanzia saa 11:15 Alasiri hadi baada ya swala ya Magharibi na Isha.
Pili: Dua-u Iftitaah kuanzia saa 02:30 Usiku.
Tatu: Muhadhara wa kidini (mawaidha) kuanzia saa 03:00 Usiku.
Nne: Mashindano ya Qur’an ya vikundi.. nayo hufanyika kila mwaka na hushiriki vikundi vya Qur’an kutoka mikoa yote ya Iraq yatarushwa kila siku kuanzia saa 06:00 Usiku. (rekodi).
Tano: Dua-u Abii Hamza Shimaaliy kuanzia saa 07:00 Usiku itaendelea hadi baada ya swala ya Alfajiri.
Fahamu kua: Dua-u Abii Hamza Shimaaliy na dua za usiku pamoja na Qur’an tukufu zitarushwa kutoka katika Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), huku kisomo cha Qur’an na swala ya Magharibi na Isha pamoja na swala ya Alfajiri zitarushwa kutoka katika Atabatu Abbasiyya, siku ya Alkhamisi itaongezwa Dua-u Kumail katika ratiba ya matangazo na siku ya Ijumaa itaongezwa Hotuba ya swala ya Ijumaa kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu.
Kwa maelezo zaidi unaweza kuwasiliana na Ustadh Bashiri Taajir kiongozi wa idara ya watalamu wa Alkafeel kwa simu namba (009647706007187) au Muhandisi wa urushaji wa matangazo Ihabu Awidiy kwa namba (009647706054144).