Kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya kimekamilisha awamu ya tano ya semina kuhusu uchunguzi wa nakala kale (makhtutwaat) zinazo nasibishwa na “aliye kua akimuhami Mtume (s.a.w.w)” semina hiyo ni sehemu ya mafunzo maalumu ambayo hutolewa kwa watumishi wa Ataba na wasio kua watumishi, kwa lengo la kujenga uelewa zaidi katika sekta hii.
Hafla ya kufunga semina hiyo ilifanyika katika ukumbi wa imamu Haadi (a.s), baada ya kusomwa Qur’an tukufu ya ufunguzi na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, rais wa kitengo hicho Shekh Ammaar Hilali alielezea nafasi ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuhuisha turathi na namna inavyo wasaidia watafiti wa turathi, alisema kua: “Lengo la kufanya semina hizi ni kuhakikisha ndugu zetu wanaendelea kufanya utafiti, na kalamu zao zinakua na uwezo wa kubaini ubora uliopo katika turathi wanazo zipata kutoka katika vituo vya turathi vilivyo chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu”.
Dokta Zamaan Ma’amuriy mmoja wa wakufunzi wa semina hii amesema kua: “Imefanyika juhudi kubwa kwa ajili ya kufanikisha semina hii, imeandaliwa selibasi maalumu inayo endana na viwango vya washiriki, tunatarajia kua tumefikia malengo na tunategemea elimu iliyo tolewa katika semina hii ifasiriwe kwa vitendo halisi”.
Kulikua na ujumbe wa washiriki wa semina hii pia, katika ujumbe wao waliishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwapa fursa ya kushiriki katika mafunzo haya muhimu kwao, na wakaomba kuendelea kufanyika kwa semina za aina hii, mwishoni mwa hafla hii walimu na wakufunzi wa semina walipewa vyeti vya shukrani na washiriki wa semina wakapewa vyeti vya ushiriki.