Mkoa wa Misaan moja ya vituo vya (matibabu bila malipo), na uongozi wa hospitali wasisitiza kua huduma walizo toa zimepunguza mateso ya wagonjwa..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ziara zinazo fanywa na jopo la madaktari wa (matibabu bila malipo) mradi unao endeshwa na hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, hivi karibuni wameingia katika kitongoji cha Mujarra ndani ya mkoa wa Misaan, kwa ajili ya kutoa huduma za kimatibabu bure kwa wakazi wa kitongoji hicho pamoja na kubaini mambo muhimu ya kiafya yanayo hitajika, zoezi hili limefanyika kwa kuwasiliana na jumuiya huru inayo saidia watu wenye matatizo katika mkoa wa Misaan.

Mkuu wa hospitali dokta Haidari Bahadeli amesema kua: “Mradi wa (matibabu bila malipo) unaendelea kutoa huduma, nao ni miongoni mwa miradi inayo simamiwa na hospitali chini ya maelekezo ya Atabatu Abbasiyya tukufu, na unapewa umuhimu mkubwa kwa sababu unasaidia sana kupunguza mateso ya wagonjwa na hutoa tiba bure kwa watu wasio weza kwenda katika hospitali za serikali, kwa ajili ya umbali au kukosa matibabu wanayo hitaji, mradi huu umepata muitikio mkubwa sana kwa mujibu wa wanufaika wenyewe”.

Akaongeza kusema kua: “Msafara huu umehusisha madaktari wa ndani na nje ya Iraq, tena madaktari bingwa wa magonjwa ya tumbo, watoto, wanawake, ngozi, mifupa na macho, wamefanikiwa kutoa huduma kwa wananchi elfu moja, hii ni moja ya ziara katika mkoa huu, tunatarajia kupanua huduma zetu hadi katika vitongoji vingine siku zijazo, kutokana na ratiba iliyo andaliwa na uongozi wa hospitali ya rufaa Alkafeel”.

Akafafanua kua: “Hii ni safari (ziara) ya kumi tangu kuanza kwa mradi huu, ziara hii imefanyika baada ya kuwasiliana na jumuiya ya kusaidia watu wenye matatizo iliyopo katika mkoa wa Misaan na kwa kushirikiana na viongozi wa Mujarra pamoja na hospitali ya kitongoji hiki”.

Wagonjwa wa kitongoji hiki wametoa shukrani kubwa kwa Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kuwapa huduma hii ya kibinadamu ambayo walikua wanaihitaji sana, na kuwapa nafasi ya kwenda hospitali na kutibiwa bure jambo ambalo sio la kawaida tena katika kiwango cha juu kiasi hiki.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: