Siku ya kwanza, Ramadhani 14/1438h.
Ufunguzi wa kongamano saa tatu jioni:
- 1- Kisomo cha Qur’an tukufu.
- 2- Kupandisha bendera ya Mkarim wa Ahlulbait (a.s).
- 3- Maneno ya ukaribisho kutoka kwa watu wa mji wa Hillah/ mji wa imamu Hassan Almujtaba (a.s).
- 4- Ujumbe wa Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya).
- 5- Qaswida ya kishairi kutoka kwa dokta Mudhwaru Almadaniy/ katibu mkuu maalumu wa Masjid Sahla tukufu.
- 6- Qaswida ya kishairi kutoka kwa Mudhwaru Aalusiy.
- 7- Maneno yanayo ashiria furaha ya kuzaliwa kwa mkarimu wa Ahlulbait kutoka kwa mtumishi wao Hameed Twawirjaawiy.
- 8- Uzinduzi wa maonyesho ya picha zilizo chorwa na vijana wa Hamza katika mkoa wa Baabil/ maonyesho ya picha za mashahidi wa Hashdi Sha’abi watukufu kutoka katika taasisi ya Ain na maonyesho ya picha za mashahidi wa Iraq kutoka katika taasisi ya kusaidia mayatima.
Siku ya pili, Ramadhani 15/1438h.
Siku ya mashairi ya kizalendo yataanza saa tatu jioni:
- 1- Usomaji wa Qur’an tukufu.
- 2- Qaswida za mazazi zitakazo imbwa na kikosi cha Qaswida za kiislamu kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu, kikiongozwa na Ustadh Ali Kadhim Mandhuur.
- 3- Kongamano la kuzaliwa kwa mkarimu wa Ahlulbait (a.s) la kishairi kwa ushiriki wa:
- A- Mshairi Muhammad A’ajibiy - kutoka Samaawah.
- B- Mshairi Zainul-abidina Saidiy - kutoka Karbala.
- C- Mshairi Hussam Hamzawiy - kutoka Baabil.
- D- Mshairi Muhammad Faatwimiy - kutoka Baabil.
- E- Muimbaji Raaid Fatalawiy - kutoka Baabil
Siku ya tatu, Ramadhani 16/1438h.
Hafla ya kuhitimisha kongamano katika malalo ya Sharifat Alawiyyah bint wa imamu Hassan (a.s).
- 1- Usomaji wa Qur’an tukufu.
- 2- Kupandisha pendera ya mkarimu wa Ahlulbait (a.s).
- 3- Maneno ya ukaribisho kutoka kwa katibu maalumu wa mazaru hiyo tukufu.
- 4- Ujumbe kutoka kwa uongozi wa juu wa mradi wa Hillah ni mji wa imamu Hassan Almujtaba (a.s).
- 5- Qaswida ya kishairi kutoka kwa Ustadh Najaah Arsaan.
- 6- Muhadhara wa kitafiti.
- 7- Kuwapa zawadi wanafunzi wa mkoa huu walio faulu darasa la sita katika shule za msingi.
- 8- Kugawa zawadi kwa washiriki.
- 9- Kufungwa kwa kongamano.
Ustadh Hassan Hilliy mkuu wa mradi wa Hillah ni mji wa imamu Hassan (a.s) alibainisha kua: “Kuna vitu kadhaa vitafanywa kabla ya kuanza kwa kongamano hili.
Siku ya Juma Tano, Ramadhani 11.
Kikao cha kuwakirim wanahabari wa kituo cha Karbala kwa kumaliza mwaka wa tisa tangu kuanzishwa kwake.
Siku ya Alkhamisi, Ramadhani 12.
- 1- Kutakua na hafla ya kumkumbuka hoja wa kiislamu Shekh Ali Samaka (q.s) na hoja wa kiislamu Shekh Muhammad Samaka (q.s) kwa kusaidiana na kituo cha turathi za Hillah chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
- 2- Mahafali ya Qur’an itakayo ongozwa na Maahadi ya Qur’an ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
Siku ya Ijumaa, Ramadhani 13.
Kutakua na hafla maalumu itakayo ongozwa na Atabatu Kadhimiyya tukufu kwa kushirikiana na uongozi wa mradi wa Hillah ni mji wa imamu Hassan Almujtaba (a.s), hafla hiyo itapambwa na kuzizawadia familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi watukufu.