Usiku wa Ijumaa wa kwanza katika mwezi wa Ramadhani watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) waongeza juhudi za kuwapokea mazuwaru..

Maoni katika picha
Siku za Ijumaa hua kuna ongezeko kubwa la mazuwaru kutoka ndani na nje ya Iraq, unapo ingia mwezi wa Ramadhani mtukufu siku hizo hua na upekee maalumu, huongezeka idadi ya mazuwaru maradufu tofauti na miezi mingine, Alasiri ya siku ya Alkhamisi yameingia makundi mengi ya mazuwaru, hii ni kwakua wengi wao wanaanza safari baada ya Adhuhuri ili wafike (haram) karibia ya muda wa Maghribaini.

Watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) kutokana na juhudi zao tukufu na kwa mujibu wa ratiba iliyo pangwa na Atabatu Abbasiyya katika mwezi huu, wamejipanga kutoa huduma bora kwa mazuwaru watukufu na kuwawekea mazingira mazuri ya kutekeleza ibada kwa utulivu, pamoja na kuwarahisishia kufanya ziara na kumuelekea Mwenyezi Mungu kwa unyenyekevu, na kuhakikisha wanapata furaha katika nafsi, miongoni mwa maandalizi yaliyo fanyika ni:

  • 1- Kutandika miswala (mazulia) eneo linalo zunguka ukumbi wa haram tukufu ili kuwarahisishia mazuwaru wengi kufanya ziara na kuswali.
  • 2- Mgahawa (mudhifu) wa Atabatu Abbasiyya tukufu unaandaa chakula kingi kwa ajili ya kuwafuturisha mazuwaru watukufu.
  • 3- Kuandaa vyakula vyepesi vya kufturu mazuwaru ambavyo ni tende, maji na supu.
  • 4- Kujaza maji ya baridi katika madeli na matenki yaliyopo ndani ya hara na yaliyopo katika njia zinazo ingia ndani ya eneo tukufu la haram.
  • 5- Kuandaa vyoo katika maeneo ya karibu na haram tukufu kwa ajili ya kutumiwa na mazuwaru.
  • 6- Kuongeza ukubwa wa eneo la kusomea Qur’an, ambayo inasomwa kila siku ndani ya haram tukufu na kuongeza idadi ya misahafu.
  • 7- Kuongeza maeneo ya kuswalia swala za jamaa za wanaume na wanawake.
  • 8- Kuandaa njia za kuingia na kutoka baada ya kumaliza kuswali jamaa.
  • 9- Kuongeza idadi ya vitabu vya ziara na vya dua pamoja na kuongeza idadi ya turba ndani na nje ya haram.
  • 10- Kuongeza idadi ya mikokoteni ya kubeba wagonjwa wasio weza kutembea pamoja na kuongeza idadi ya magari yanayo tumia umeme kwa ajili ya kusaidia kubeba watu hasa wazee.
  • 11- Kuongeza idadi ya machapisho ya Alkafeel na Alkhamisi na kuyagawa bure kwa mazuwaru watukufu.

Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya siku ya Alkhamisi ya mwezi tano Ramadhani zilishuhudia ongezeko kubwa la watu wanaokuja kufanya ziara (mazuwari) na ilifikia kilele cha mafuriko ya watu hao karibia na muda wa Maghribaini.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: