Miongoni mwa maandalizi ya vita ya Tal-afar na kusaidia upatikanaji wa siraha za kivita za ndani, kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kupitia watalamu wake wa kiwanda cha siraha cha Basra, wametengeneza bomu walilo liita (Radi/1) linalo kidhi sifa zote za vifaa vya kivita na lenye ubora mkubwa ambalo linaongezwa katika hazina ya siraha za kujilinda na kushambulia, baada ya kufanyiwa majaribio siraha hiyo imethibitika kua ni siraha bora zaidi katika siraha zilizo tengenezwa hapa nchini na inatoa ushindani mkubwa kwa siraha zinazo agizwa nje ya nchi.
Kifaa cha Raajimah (kurushia mabomu) kina uzani wa (mm 240) tofauti na Raajimah zilizopo katika makundi ya Hashdi Sha’abi ambazo zinategemea kifaa cha kirusi chenye uzani wa (mm 122), haya ni mafanikio makubwa kufikiwa hapa Iraq kwa mara ya kwanza, mabomu hayo yanauwezo wa kufungwa vichwa vikubwa hadi vya uzito wa (kilo 250), umabali unao weza kushambuliwa na mabomu haya bado ni siri hadi hivi sasa, kifaa cha Raajimah kinaweza kufungwa katika gari la “International” na katika deraya, yamethibitisha uwezo wake, inaweza kufungwa Raajimah yenye kubeba mabomu nane yenye kishindo cha (tani 2), mabobu yote nane yanaweza kurushwa kwa (sekunde 16) takriban.
Bado kinaendelea kufanyiwa kazi (matengenezo) kifaa cha Shihaab (siraha nyingine ya kivita) ipo katika hatua za mwisho ambayo inatarajiwa kukamilika hivi karibuni.