Hakuna shaka kuhusu baraka za mwezi wa Mwenyezi Mungu mtukufu mwezi wa Ramadhani kiroho na kimazingira zimeenea muda wote na sehemu zote, kwa dalili ya kauli ya imamu Baaqir (a.s) isemayo: (Kila kitu nina malkia na malkia wa Qur’an ni mwezi wa Ramadhani), toka kuingia kwa mwezi huu mtukufu roho zimejaa imani na zinajituma kuisoma Qur’an na kurekebisha makosa yao pamoja na kusafisha kutu ndani ya nyoyo zao zilizo sababishwa na madhambi waliyo tenda.
Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia maelekezo yake kuhusu Qur’an tukufu na kuandaa kizazi chenye kufuata mafundisho ya Qur’an ambayo ndio msingi wa uislamu na kitabu ambacho kinatakiwa kujulikana zaidi katika jamii, haiwalengi wanaume peke yao bali kuna juhudi maalumu za kuwahusisha wanawake pia, kupitia Maahadi ya Qur’an tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu, matawi yao yameenea katika mikoa ya Iraq, yanaendesha harakati kuhusu Qur’an na kipao mbele chao ni kuendesha visomo vya Qur’an tukufu, kwa ushiriki wa makundi ya wanawake wakiongozwa na kina dada mahiri katika usomaji wa Qur’an tukufu, visomo hivyo vinafanywa kila siku ndani ya mwezi huu mtukufu.
Kumbuka kua lengo la kufanyika kwa visomo hivi ni kwa ajili ya kueneza tamaduni za Qur’an na mafundisho halisi ya Mtume Muhammad (s.a.w.w) na kutambulisha mafundisho ya kiislamu amboya yanahitajika zaidi katika jamii wakati huu.