Shamba boy wa Alkafeel wafungua kituo kipya cha kuuza maua na wasisitiza kua wanaweza kutosheleza mahitaji ya mkoa huu na mingine pia..

Maoni katika picha
Jopo la wafanya kazi wa shamba boy wa Alkafeel chini ya kitengo cha utumishi katika Atabatu Abbasiyya tukufu wamefungua kituo kipya katikati ya mji (katika barabara ya Jamhuriyyah) cha kuuza maua. Kiongozi wa shamba boy hao Ustadh Muayyad ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hakika kituo hiki ni moja ya vituo vilivyo pangwa kufunguliwa katika mkoa wa Karbala katika hatua ya kwanza, na katika hatua nyingine tutafungua mikoani, jambo hili limefanyika baada ya shamba boy wa Alkafeel kuotesha mimea (maua) ya msimu na ya kudumu, ya aina mbalimbali miongoni mwake zikiwemo aina kutoka nje ya Iraq zinazo endana na hali ya hewa ya hapa nchini, zipo aina ambazo zimeoteshwa kwa wingi katika vitalu na zipo tayari kuuzwa”.

Akaongeza kusema kua: “Kwakua vitalu vipo nje ya mji jambo linalo sababisha usumbufu kwa wateja kwenda katika vitalu hivyo ndio maana tumeamua kuwarahisishia kwa kufungua kituo hiki katikati ya mji, hii ni miongoni mwa juhudi za idara kuwaondolea wateja usumbufu wa muda, ubebaji na mengineyo, hivyo ikaonekana kua njia hii ndio njia nzuri ya kuwarahisishia wateja wetu wa ndani na nje ya mkoa wa Karbala tukufu”.

Kuhusu wasifu wa kituo hicho Ustadh Muayyad alisema kua: “Kituo kimejengwa katika eneo lenye ukubwa wa mita za mraba 120 na kimesanifiwa vizuru kwa ajili ya maonyesho, tumeweka aina tofauti za mazao yetu, miti, mimea, maua ya msimu na mengineyo, baada ya kuandaa mazingira mazuri na kila aina kutengewa sehemu yake maalumu, hali kadhalika katika kituo hiki kuna sehemu ya kuonyeshea asali ya nyuki tunayo zalisha pamoja na sehemu ya kuonyeshea mbolea inayo zalishwa na kiwanda cha Aljuuda kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu. Kuanzishwa kwa kituo hiki kumezingatia mambo mengi miongoni mwa mambo hayo ni: “Ubora wa sehemu, imechaguliwa sehemu ya katikati ya mji (barabara ya Jamhuriyyah) ambayo ni moja ya barabara zilizo karibu na Atabatu Abbasiyya tukufu na imeungana na barabara za mji wa Karbala wa zamani, ni sehemu rahisi kufikika, mteja anaweza kufahamu kila kinacho zalishwa katika vitalu vyetu pamoja na bei kupitia kituo hiki, iwapo mteja atahitaji kitu chochote ataletewa kutoka vitaluni moja kwa moja”.

Mwishoni mwa maongezi yake Ustadh Muayyad alisema kua: “Shamba boy wa Alkafeel wapo tayali kuandaa mimea kadri inavyo hitajika hapa Iraq kwa ajili ya kupandwa katika barabara na sehemu za bustani kwa bei nafuu kabisa tofauti na kuagizwa kutoka nje ya nchi, tena mimea inayo weza kustahamili hali ya hewa, hali kadhalika wananchi wa ndani na nje ya mkoa huu wanaweza kuja kununua moja kwa moja katika kituo hiki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: