Mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wafuturisha mayatima..

Maoni katika picha
Kutokana na malengo ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya kuitumikia jamii na kuwapa furaha watoto mayatima pamoja na familia zao hasa katika siku hizi za mwezi mtukufu wa Ramadhani, mgahawa wa Abulfadhil Abbasi (a.s) umewafuturisha mayatima na wajane ndani ya ukumbi wa mgahawa huo, hii ni sehemu ya ratiba ya mwezi huu mtukufu na inafanyika chini ya utaratibu maalumu kwa kusaidiana na kuwasiliana na kamati inayo husika na watu hao.

Program hii ni miongoni mwa mambo muhimu yanayo fanywa na kitengo cha mgahawa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, inayo lenga kujenga mapenzi na mawasiliano na kundi hili la mayatima na wajane –hususan mayatima wa mashahidi wa Hashdi Sha’abi na wa jeshi la serikali- kwa ajili ya kuwafanya wahisi kua wana uangalizi, na kuwafanya wapate furaha katika nyoyo zao. Tunatoa wito kwa kila aliye soma dini ya kiislamu achangie katika kufanikisha juhudi hii iliyo anzishwa na Atabatu Abbasiyya katika mwezi huu mtukufu.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalumu katika mwezi huu wa Ramadhani na miongoni mwa vipengele vya ratiba hiyo ni jambo hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: