Watumishi wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) wamepata utukufu wa kumtumikia yeye pamoja na dada yake bi Hauraa (a.s)..

Maoni katika picha
Kutokana na maelekezo ya kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i) ugeni wa watalamu ambao ni miongoni mwa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wamefanya marekebisho mbalimbali katika malalo ya bibi Zainab (a.s) katika mji mkuu wa Syria Damascus, hii ni kwa sababu malalo hayo yalikua yanahitaji kurekebishwa kutokana na uadui yanao fanyiwa na magenge ya kigaidi yanayo sumbua katika nchi hiyo, kutokana na hali tete ya usalama imepelekea kuchelewa kufanyiwa marekebisho jengo hilo.

Ugeni uliongozwa na rais wa kitengo cha utunzaji wa Haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Hassan Hilaal ambaye amesema kua: “Tumewafikishwa na umekua utukufu mkubwa kwetu kufanya marekebisho katika baadhi ya sehemu ya malalo matukufu ya bibi Zainab (a.s), tumehakikisha tunazifanya sehemu hizo kua na muonekano mzuri zaidi, tumetumia uwezo wetu wote kwa ajili ya kufanikisha jambo hili”.

Akaongeza kusema kua: “Kazi ilianza baada ya upembuzi yakinifu wa aina ya marekebisho yanayo hitajika katika malalo hii tukufu, baada ya kubaini marekebisho yanayo hitajika kazi ilianza mara moja kwa kugawa majukumu kwa watumishi walio kua na hamu kubwa ya kutekeleza majukumu hayo, kazi ilikua kama ifuatavyo:

Moja: Kufunga spika katika eneo lote la haram tukufu na maeneo yanayo izunguka zenye usikivu mzuri.

Pili: Kusafisha kubba tukufu la malalo ya bibi Zainab (a.s), ukizingatia kua watalamu wetu wana uzoefu mkubwa katika kazi hiyo, walianza kulisafisha baada ya kuondoa udongo uliokua juu ya kubba hilo.

Tatu: Kusafisha dirisha la kaburi tukufu na pembezoni mwake kwa kuondoa aina zote za uchafu.

Nne: Kusafisha milango yote ya malalo tukufu.

Tano: Kusafisha na kurekebisha mapambo.

Sita: kusafisha maraya za haram tukufu.

Kumbuka kua kazi hii ilidumu kwa siku kadhaa, na watalamu wetu walifanya kazi usiku na mchana ili kulifanya eneo hili tukufu liwe na muonekano bora zaidi, walio fanya kazi hii waliteuliwa na uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ukawatunuku utukufu wa kuhudumia malalo mbili tukufu, malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na malalo ya dada yake bibi Zainab -Al-aqilah- (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: