Scuot wa Alkafeel waendesha ratiba ya kwanza ya Anwaari Mahdi ya kisomo cha Qur’an ndani ya mwezi wa Ramadani..

Maoni katika picha
Katika mwezi huu wa Ramadhani, na kutokana na ratiba iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa vitengo vyake vyote kwa ajili ya kuhuisha siku hizi tukufu, Jumuiya ya Scuot ya Alkafeel chini ya kitengo cha watoto na makuzi ndani ya kitengo cha habari na utamaduni kwa mara ya kwanza wanaendesha ratiba maalum katika mwezi huu mtukufu.

Kiongozi wa ufungaji wa mahema bwana Ali Hussein Abduzaid aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kwa ajili ya kutekeleza ratiba ya Mwezi wa Ramadhani inayo endana na kipindi cha likizo za majira ya kiangazi, tumeanza kufanya harakati kadhaa miongoni harakati hizo ni ratiba hii ambayo tunatarajia kufanikisha malengo yetu”.

Akaongeza kusema kua: “Ratiba hii inalenga kutoa mafunzo kwa wanachama wa Scuot na kuwaendeleza katika kutambua Qur’an pamoja na kuongeza uwezo wa kuitafakari, na kunufaika na nguvu ya ujana waliyo nayo pamoja na kutumia vizuri muda wao”.

Akabainisha kua: “Ratiba hii imebeba vitu vingi, imepangwa kutokana na uwiyano wa umri wao na elimu zao, miongoni mwa vitu hivyo ni:

Moja: Mashindano.

Pili: Mafunzo ya kazi ambapo kuna nadhariya na vitendo.

Tatu: Mihadhara kuhusu Qur’an, Fiqhi na Aqida.

Ratiba hii pia ina vipindi vya masomo, na imepata muitikio mkubwa sana kutoka kwa washiriki, kwa sababu ratiba yake ni nyepesi na mambo yaliyomo yamewavutia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: